GET /api/v0.1/hansard/entries/1499515/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499515,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499515/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nami nichangie Mswada huu ulioletwa hapa na dada yetu Mhe. Irene, tunayempongeza sana. Irene, twajua kazi unaitenda. Mwenyezi Mungu ndiye mbunifu kushinda watu wote. Naye hakutupa mti ule kwa kuwa alijua hauna umuhimu kwetu. Wakati mwingine tunaleta ufundi lakini Mwenyezi Mungu amepanga mambo kwa mipango yake. Amepanga bila kubagua au mapendeleo. Kwa mfano, tuna Mikoko, Mikoma na mazao mengine Mwenyezi Mungu mwenyewe alitupangia katika Kaunti ya Lamu. Alijua kuwa aina hii ya miti inakua vizuri sehemu hii, wala siyo jukumu langu mimi mkaazi wa Lamu nipange mambo yetu ya kibinadamu. Huenda nikataka kuleta kitu ambacho pengine ni kizuri kwingine lakini hakiwezi kunawiri huku. Mimi mwenyeji wa Lamu ninaweza kusema ninataka kupanda mchai ama mkahawa. Itawezekana vipi? Kwa hivyo, mti huu uitwao mkaratusi haufai."
}