GET /api/v0.1/hansard/entries/1499520/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499520,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499520/?format=api",
    "text_counter": 383,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Iwapo mti huu una shida, basi ni kwa vile umeletwa na binadamu. Nimejulishwa kwamba mti huu haukuwepo Kenya. Ulikuwa ni wa kwingine. Maji ni mhimu. Kukiwa na mti unaokunywa maji zaidi, basi unafaa kuondolewa. Sisi binadamu tuna vita na wanyama kwa sababu ya maji. Hayo maji ni muhimu kwa mazingira, kwetu sisi binadamu, na wanyama kwa jumla. Kuna haja ya kuharakisha hili suala. Sasa hivi kuna Waziri mtendakazi kwenye Wizara husika, Insh’Allah. Kulikuweko Waziri mwingine mtendakazi kule. Insh’Allah, wote walifanya kazi nzuri. Najua tutasaidika. Tuko pamoja naye kurekebisha. Iwapo huu mti waafaa kutolewa, bila shaka utolewe na usipandwe kabisa. Tupande miti yenye faida na inayokubalika katika maeneo. Kule kwetu kuna mti mbadala wa aina ya Kasorina. Si lazima tupande hii e ucalyptus ambayo ina athari nyingi. Tunasikia uchungu zaidi kutokana na athari hizo. Katika Kenya nzima, wakaaji wa Lamu wafaa kupongezwa zaidi. Nyeri ndiyo kaunti yenye miti nyingi zaidi kisha Lamu ni ya pili. Tunajivunia kuhifadhi mazingira. Naunga mkono kuwa mti huo unasumbua. Tuhakikishe kuwa Mswada huu umepita. Wizara pia yafaa isaidie ili hili jambo lirekebishwe. Asante."
}