GET /api/v0.1/hansard/entries/1499580/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499580,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499580/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Pia najua Kamati ya Sheria iliyokabidhiwa nao pia wamejifunza mengi. Kama kuna mambo yatakayohitaji kutunga sheria zaidi za kulinda gatuzi, najua Kamati hii ya Seneti itatuelezea. Bunge la Kaunti ya Taita Taveta lilikuwa liwe mwenyeji wa Seneti Mashinani huu mwaka. Tulikuwa tunashindana na Kaunti ya Busia. Lakini changamoto iliyokuwa pale ni ya nafasi ya Bunge la Kaunti ya Taita Taveta kuwa ndogo. Lakini nafurahia na Kaimu Spika yuko pale ya kwamba Kaunti ya Taita Taveta wameanza kujenga Bunge lingine. Najua katika siku za usoni, wakati tunaangalia kaunti ya kwenda, basi Taita Taveta itakuwa ni mmojawapo za kaunti za kupeleka Seneti Mashinani. Karibuni sana wawakilishi wa Bunge la Kaunti ya Taita Taveta. Mkirudi nyumbani, muwasalimie watu wa nyumbani. Asante, Bw. Spika."
}