GET /api/v0.1/hansard/entries/1499620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499620,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499620/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Ndio maana mara nyingi unaona polisi wengi wakiwa na matatizo ya kiakili. Hilo ni jambo la maana sana. Polisi wanapohamishwa kutoka sehemu moja kupelekwa nyengine, wanafaa kuridhika na mahali wanapopelekwa na wapewe ridhaa ya kukaa mahali pale. Jambo la pili ni kuhusu Taarifa iliyoulizwa na Seneta wa Kaunti ya Murangá. Katika kikao kilichoisha katika Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ambacho mimi ni Mwenyekiti, tulikaa na Waziri na kumwambia kwamba angeongeza makataa ili macadamia iuzwe kwa nchi za ng’ambo. Lakini tangu makataa ilipoisha tarehe mbili, mwezi wa kumi na moja, hakuna jambo limefanyika hadi sasa. Bw. Spika, wakulima wanafaa waruhusiwe kufuga mbuzi wao mahali wanaona kuna nyasi. Hizi sheria nyingi zinazoletwa zinawahadaa na kuwakandamiza wakulima. Kuna mazao mengi katika nchi hii ambayo hayana sheria, kwa mfano, mahindi na maziwa. Lakini wakulima wa korosha, macadamia na bixa wana sheria kandamizi zinazowazuia wakulima kuuza mazao yao. Asante sana, Bw. Spika."
}