GET /api/v0.1/hansard/entries/1499627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499627,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499627/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kuchangia kuhusu macadamia na mimea ambayo hutoa mafuta. Mimi nataraji kwamba Serikali kabla haijaamua ama kukata kauli kuhusiana mmea wowote nchini, lazima washika dau wote wahusishwe katika mchakato mzima. Haiwezekani kwamba Waziri ama viongozi katika Wizara, wataamka asubuhi na mapema kupitisha sheria ambayo inamgandamiza mkulima wa makandamia nchini. Haiwezi kuwa wanakata kauli kuboresha pesa ambazo mabwenyenye wanapata kuliko kuangalia hali ya maisha ya mkulima wa makandamia nchini. Mimi na mwenzangu mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi samawati, hivi karibuni tutamkaribisha mheshimiwa Waziri kuweka bayana kile kilichosababisha kuwanyima wapandaji ama wakulima wa makandamia nafasi ya kupata kipato kwa jasho lao. Changamoto nyingine ambayo ipo katika wizara hii ni wakulima wa ngano. Haiwezekani wapatie kibali mabwenyenye kuagiza ngano kutoka nchi ya nje na wakulima wa ngano katika Bonde la Ufa na pembe mbalimbali nchini wako na ngano katika maghala yao. Hii ni hali ambayo sisi kama maseneta hatuwezi kubali. Lazima Serikali iweke Wakenya wakulima mbele pasipo kuweka kiu cha pesa kwa njia ya mkato. Asante sana, Bw. Spika."
}