GET /api/v0.1/hansard/entries/1499648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499648,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499648/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, ningependa kuchangia taarifa iliyoletwa na Sen. Munyi Mundigi wa Kaunti ya Embu. Kwa hakika, ni jambo la kutamausha kuona kwamba hali ya maisha na mazingira ya askari wetu ni ya kusikitisha sana kwa sababu ni mabaya. Tukirejea nyuma, tumekuwa na azma nzuri. Maseneta wengi wamezungumza kuhusu mazingira wanayoishi askari wetu lakini wanasahau azma ambayo Rais wetu William Samoei Ruto alikuwa nayo wakati wa kampeni inayoendelea kutekelezwa. Kuna swala la nyumba za bei nafuu ambazo zinajengwa kwa minajili ya kuwapa askari mahali pazuri pa kuishi na familia zao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}