GET /api/v0.1/hansard/entries/1499676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499676,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499676/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa ruhusu nichangie mjalala utakuako wakati wa siasa. Ninapinga Mswada huu kwa sababu hapa Kenya kila kitu kinafuata demokrasia. Wakati tutapitisha huu Mswada kutakuwa na shida kwa sababu kuna matajiri na masikini. Kila mmoja atakuwa anataka kiti ya ubunge, kaunti au Seneta ili asimame. Unaweza pata watu wengine wamekuwa wagonjwa. Kuna watu wako na pesa, watawasimamia hao wagonjwa ambao hawana pesa. Kwa hivyo, ninapinga huu Mswada sababu watu watakuwa wanatafuta barua ili waweze kufanya harambee. Kwa sababu nchi ya Kenya ina demokrasia, inapaswa tuwe na uhuru wa kila kitu upande wa siasa. Ule hana pesa atajua vile ataomba pesa kutoka kwa wale wako na pesa na ule anataka kuchangiwa atajua vile atafanya ili tuweze kusaidia wananchi wa Kenya. Tunajua ikija mambo ya siasa, hatuna ubaya na mtu yeyote, aliye na pesa na ule hana na kuchangisha iwe huru."
}