GET /api/v0.1/hansard/entries/1499681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499681,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499681/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi kutoa maoni yangu kuhusu Mswada ambao unahusika na mambo ya harambee. Harambee hapa Kenya zimekuwa na shida. Katika historia ya Kenya, Mzee Jomo Kenyatta aliweka Wakenya wote pamoja kwa mwito wa harambee. Harambee ni jina liko na msingi wa Kihindi ambao unasema kuvuta pamoja. Ukweli wa mambo, hili lilikuwa wazo nzuri sana na limesaidia watu wengi katika Kenya hii. Shida imekuwa kwamba, kuna wengine wametumia nafasi hiyo vibaya. Ni kweli kuna watu ambao wametumia harambee vibaya. Kwa mfano, tunasikia wewe ni mheshimiwa ama ni kiongozi wa tabaka fulani, umeenda mahali kuomba mwenyezi Mungu na hukwenda kwa mambo ya harambee, lakini hapo hapo, watu wanajipanga na mara unaanza kuambiwa, kuna shida hii na ile. Kwa hivyo, mheshimiwa au mtu fulani ukiwa unaondoka, ujue kuna haya. Bw. Spika, ni kweli kwamba, kuna watu ambao wamekuwa wakitumia nafasi hii ya harambee hizi kutekeleza mambo yasiyo ya kisawa na mabaya. Pia wakati mwingine tumesikia tunafanya harambee halafu pesa hizo hazitumiki kwa ile mipangilio harambee hiyo ilifanywa. Harambee inafanyika na watu waliokusanya zile pesa, hawajui ni pesa ngapi zilipatikana na hizo pesa zinatumika namna gani. Watu wamekuja kuelewa kuwa harambee ni namna fulani ya kusukuma mawazo ya watu kuelekea pale wanataka. Sheria hii inasema kwamba viongozi walio mamlakani na tabaka fulani, wasifanye harambee. Nimeangalia huu Mswada na nikaangalia watu wetu wa Tana River. Nitasema kwetu sisi Tana River, watu wetu wanaotuita harambee, wanatuita kwa sababu ya shida. Kama wewe ni kiongozi na sio lazima uwe ni mheshimiwa, kuna walimu, madaktari na wafanyi biashara mashuhuri ambao pengine mwenyezi Mungu amewafungulia neema zake. Sasa watu wakiwa na shida, pengine mtu amepata ajali, mtoto au bibi yuko hospitali, ama pengine ni ugonjwa na watu hawana bima. Wamezoea kwamba, kifo kikikupata, unatafuta familia yako. Familia yako inaona hiyo pesa wamekusanya haitoshi na mazishi yako bei ghali. Hii ni kwa sababu, ni lazima watu wale, mwili utolewe kutoka"
}