GET /api/v0.1/hansard/entries/1499683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499683,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499683/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "uletwe, watu walale usiku. Kule kwetu, watu wanaimba nyimbo usiku mzima, halafu asubuhi, ndio watu wanaenda kanisani. Bw. Spika, ukiniambia mimi kama Seneta wa Tana River ya kwamba, leo nipige kura ama nizungumzie Mswada ambao unasema nisisaidie watu wangu, siwezi kubaliana na wewe kabisa. Ninaomba Bunge letu hili la Seneti tuwache mambo yawe wazi. Ikiwa wewe unaona hutaki kufanya harambee, basi usifanye harambee. Ikiwa unaona wewe unaona mtu amekufa na watu wana shida pale na unaweza saidia, wasaidie. Unaweza kufanya harambee ya wagonjwa, wasaidie. Watoto wamekwama shule, bursary ndio hizi hazipatikani, msaidie kwa njia ya harambee. Watoto wengine wanaambiwa waende shule kwanza ndio wapate bursary. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}