GET /api/v0.1/hansard/entries/1499684/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499684,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499684/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tafadhali, kama mtu amepata nafasi na Mwenyezi Mungu amemubariki hata kama ni kwa uchache, yeye ni mwalimu mkuu mahali, mfanyabiashara, District Officer (DO), District Commissioner (DC) ama yeye ni Mbunge wa kaunti, Seneta, Bunge la Taifa au Waziri; kwa nini tuwafungie baraka zao? Sisi tunafundishwa katika Biblia ya kwamba mtu anayetoa anabarikiwa. Kwa hivyo, kama kuna nafasi ya kupata baraka zile za Mwenyezi Mungu, kwa nini tusizipate? Bw. Spika, mimi naomba sana tusipitishe sheria ambazo ziko kinyume na matakwa ya wananchi wetu. Sijui hapa mjini kuko namna gani. Pengine hapa mjini watu wako na pesa. Pengine hawataki kufanya harambee. Lakini sisi tunaishi na hizi shida. Wabunge wetu wa kaunti kule wanasema, “Mheshimiwa nisaidie. Nimezidiwa.” Sasa kama Mbunge wa Bunge la Kaunti anakuambia umsaidie, halafu unakataa eti tumepitisha sheria, wananchi hawataikubali sheria hii kwa sababu wananchi ndio wanatuambia tuwasaidie. Sio jambo la uwongo ama ujanja. Wale tunaoenda kwa kaunti zetu, tunapata kuwa nyumba nyingi watu wako na shida. Watu hata chakula hawana. Umeenda kutafuta chakula huko na umevamiwa na nyati ama umeumwa na mamba huko mtoni halafu mtu anakuambia eti kuna sheria inasema huwezi kwenda kwa Member of the County Assembly (MCA) ama Mbunge wako umuombe msaada. Mimi sioni kama hii sheria itatusaidia. Haisemi mambo ya wananchi. Nataka kueleza hivi. Kuna sheria ambazo tumepitisha hapa Kenya ambazo baadaye tumekuja kujuta. Kuna sheria ambazo zinasukumwa na watu fulani kama hizi NGOs. Wanasukuma sheria fulani eti tufanye hivi ndivyo dunia inavyoenda. Halafu hizo sheria haziambatani na matakwa ya wananchi waliotuchagua hapa. Halafu baadaye kidogo unaona sheria hizo zinaanza kutupiga kule mashinani. Hakuna haja kupitisha sheria ambayo itasema kama mtu ako na nafasi ya kusaidia na mwenzake amekuja ameweka mchango, hatuwezi kumsaidia. Kwa hivyo, huu Mswada kama ni kuupitisha lazima ufanyiwe marekebisho ya kuwapa watu nafasi. Iwapo kuna pingamizi yoyote au shida yoyote, irekebishwe. Lakini kusema ya kwamba eti Maseneta, Mawaziri, walimu, naibu kamishina wa kaunti, madaktari na wengineo, kwa sababu umeajiriwa na Serikali, huwezi kushiriki katika harambee usaidie wananchi wako, mimi sioni kama hilo ni wazo nzuri. Ninaomba Seneti tuuangalie huu Mswada, tuujadili vizuri na tuuelewe. Tusije tukapitisha sheria ambayo ukirudi nyumbani, unaenda kutandikwa nayo. Kwa hayo mengi, in principle, mimi siukubali huu Mswada. Nataka Mswada ambao utatupatia nafasi wale wanaoweza kutoa watoe wapate baraka zao; wale ambao hawana uwezo, Mungu atawasaidia waendelee nazo. Lakini kuzuia mtu, mimi sipo hapo. Bw. Spika, asante kwa nafasi hii ya kueleza mawazo yangu."
}