GET /api/v0.1/hansard/entries/1499686/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499686,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499686/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "lakini wakati ulipokuwa kiongozi, haukuzungumzia vile atakavyotibiwa kwa hospitali ambazo hazina madawa. Sheria tunayotaka kubadilisha ni kutoa ufisadi tunaposaidia watu masikini kwa sababu wakati tunasaidia wao, tunajifanya kuwa tunawasaidia lakini hatusuluhishi zile shida ambazo nchi yetu iko nazo. Kwa hivyo, ndugu zangu wale mko hapa, nakubaliana na nyinyi ya kwamba mnaweza kufanya amendment kwa Mswada huu. Lakini naomba niwaambie hivi: Sisi ndio tumeharibu uongozi wa nchi yetu. Sisi ndio wafisadi wakubwa na sisi ndio wanafiki wakubwa.” Barabara zetu ni mbaya. Hospitali zetu hazina madawa. Hakuna maji katika nyumba zetu. Halafu ukisikia mtu ni mgonjwa unasema tumia huyu jamaa pesa, basi anakufa na tutamzika. Ningependa kuwauliza nyinyi viongozi hapa huu Mswada uendelee vivyo hivyo ili tutoe ufisadi dhidi ya kusaidia mtu maskini. Ukitoa pesa kwa kanisa au kwa mchango, tumia mpesa na useme hizo pesa ulizitoa wapi ambayo umenitolea kwa sababu nimefariki; wakati nilipokuwa mgonjwa, hakukuwa na madawa. Asante, Bw. Spika."
}