GET /api/v0.1/hansard/entries/1499708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499708,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499708/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kutishia kwa kiwango ambacho wanatoa katika harambee zile kwani ni cha juu. Viongozi wengi ukiangalia mshahara ambao tunapokea kama maseneta, wabunge, magavana, makatibu na mawaziri hailingani na kiwango ambacho wanatoa katika harambee hizi. Ndiposa mori ama hasira ikawajaa Gen Z na wakasukuma kwamba lazima kuwe na sheria ya kudhibiti harambee hizi. Bi. Spika wa Muda, ningependa kukueleza kuwa hatua hii ya kupitisha sheria ya kudhibiti harambee, wazungu husema ni knee-jerk reaction. Kwamba ni magoti juu kama ninavyoelezewa hapa nyuma. Haitoi suluhu ya tatizo hili. Leo hii mimi ni Seneta maalum. Ninawakilisha vijana na natokea Kaunti ya Kwale. Kila kukicha simu yangu ya rununu, simu ya mke wangu ya rununu, simu ya"
}