GET /api/v0.1/hansard/entries/1499710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499710,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499710/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "na hata wazazi wangu hupata jumbe za kwamba kuna mchango mahali. Kwamba kuna mgonjwa anahitaji matibabu. Mimi kama kiongozi ambaye nimeteuliwa, sijapigiwa kura ama kutaja kuwa nataka kuwania nyadhifa yoyote katika kaunti yangu ya Kwale. Lakini kwa sababu wananchi wa Kwale na wa Kenya kwa ujumla wana taabu, shida na kutamani kupata msaada kutoka kwa viongozi wao unapata jumbe zile za kukualika katika harambee mbalimbali, kuchangia karo ama ujenzi. Pale eneo Bunge la Kinango mahali panaitwa Kwa Kadogo kuna jamii imenifuata mara nyingi wakiomba msaada wa kutengeneza choo cha umma, ambacho ni jukumu la serikali ya kaunti. Lakini serikali ya kaunti haiwezi kufanya kila kitu kwa sababu ya uhaba wa fedha na mipangilio. Kwa mfano, ikiwa wananchi wetu wanahitaji choo cha umma cha shilingi 70,000 au 100,000 na wamemfuata kiongozi wao aweze kuongoza shughuli ya harambee ili mradi ufanyike na jamii nzima isaidike kijumla, sio tu kwa leo, kesho wala mtondogoo bali kwa siku nyingi zijazo, sioni makosa. Bi. Spika wa Muda, ni kinaya kuwa sheria hii inampa mtu binafsi ambaye ni Waziri wa Serikali kuu na serikali ya kaunti nguvu kupita kiasi katika hali ya kudhibiti suala la harambee. Tusiwe Bunge la kutunga sheria ambazo zitatufinya sisi kama viongozi. Lazima tuketi na kuulizana wapi kuna shida. Ikiwa tunafanya harambee nyingi kwa sababu ya ugonjwa, basi Serikali, kama serikali zilizopita, inafaa kufanya juhudi za kutafuta suluhu na kuhakikisha kwamba kila Mkenya anaweza kupata matibabu bila dhiki ya kuuza mali yake au kufanya harambee. Nataka nishukuru Serikali kwa ule mfumo wake---"
}