GET /api/v0.1/hansard/entries/1499738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499738,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499738/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Napinga vikali Mswada huu. Kipengele cha 13 (1) na (2) kinasema kwamba mtu yeyote anayefanya kazi katika ofisi ya umma haruhusiwi kujihusisha kamwe na shughuli za harambee. Vile vile, mtu yeyote anayewania kugombea kiti chochote miaka mitatu kabla ya uchaguzi mkuu haruhusiwi kufanya harambee. Ni kinaya kwa sababu shughuli yote ya uongozi ni kuweza kusaidia jamii yako. Mtu asikueleze eti kwa sababu kuna hundi kutoka National Government- Constituencies Development Fund (NG-CDF), National Government Affirmative Action Fund (NGAAF), ama gavana atakuwa na fedha kutokana na Mswada ambao tumepitisha leo, nafikiri takriban milioni 387--- Naipongeza Kamati ya Mediation kwa kufanya vile. Haimaanishi kuwa ukipewa pesa hizo na una jukumu la kutoa bursary, basi huwezi kwenda kwenye mfuko wako kibinafsi ili kusaidia jamii yako. Nafikiri huo si uongozi halisi. Sisi wapwani tunasema kuwa kuna kutoa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. Ukitoa, haimaanishi wewe ni tajiri. Kuna msemo unaosema; kutoa ni moyo wala si utajiri. Ukichanga, unakuwa umeunda sadaka yako kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu kuna maisha ya dunia na ahera. Sioni haja ya kuweka sheria kumdhibiti kiongozi kama vile Sen. Mungatana ambaye yuko tayari kusaidia watu wa Tana River. Sisemi kuwa yeye ni tajiri. Mimi nimeteuliwa na niko tayari kusaidia watu wa Kwale katika michango, iwe ni harambee kuhusu mambo ya afya au kujenga kanisa. Wikendi hii, nitaenda Lunga Lunga Catholic Church kufanya mchango ambao wamenialika kwa sababu mimi ni mkristo mkatoliki na nina imani. Bibilia inasema kwamba, tukija pamoja, Yesu yu ndani yetu na kwamba, ni jukumu langu kama kiongozi kujenga hekalu la Mwenyezi Mungu. Vile vile, nimealikwa katika harambee Guro kujenga kituo cha afya, ambayo siyo jukumu langu. Kwa sababu mimi ni kiongozi, siwezi sema kuwa siwezi ingawaje sina fedha ya kufanya huo mchango. Lakini kuna marafiki ambao wameenda shule, ni wafanyi biashara, Mwenyezi Mungu amewabariki na wapo na nia ya kuregesha mkono katika jamii zao. Bi. Spika wa Muda, sio sawa kuleta sheria ya kudhibiti mtu ambaye yuko tayari kutoa. Nimesema kutoa ni moyo wala sio utajiri. Napinga vikali Mswada huo. Shukrani na Mungu awabariki."
}