GET /api/v0.1/hansard/entries/1499803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499803,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499803/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru Kiongozi wa Walio Wengi kwa sababu ya wazo nzuri. Mswada huu ni wa maana sana. Katika maisha yangu ya awali nimekuwa mwakilishi wa wadi na pia nilikuwa Kiongozi wa wengi katika Kaunti ya Kirinyaga. Kwa hivyo, naelewa masaibu yanayowafikia mawakilishi wadi ama MCAs ambao ni mengi. Kama kuna viongozi ambao wanachukuliwa kwa urahisi, mashinani wako na watu kila siku, wanaobeba mizigo, ambao inafaa wasaidiwe ni wawakilishi wadi ambao ni MCA. Mimi nilihudumu kwa kipindi cha miaka tano; kuanzia mwaka wa 2017 hadi 2022. Katika kile kipindi bado nilikuwa na marafiki wengi. Kulikuwa MCA kutoka Tebere na wengine ambao walikuwa. Tunapoongea hivi sasa, kuna MCA wawili; mmoja wa Baragwi anaitwa David Mathenge, kijana mtanashati na mwingine ambaye anaitwa David Wangui ambaye ametoka Mutira. Hawa ni mojawapo wa wawakilishi wadi ambao hivi sasa wako katika muhula wa tatu. Wanapomalizia muhula huu watakuwa wamehudumia wananchi kwa miaka kumi na tano. Lakini uchungu ni kwamba baada ya kazi ngumu ya kuhudumia wananchi, viongozi wale wataenda nyumbani mikono tupu bila kuwekeza pesa zozote katika idara yoyote ya kuhakikisha kwamba watapata fedha ya uzeeni. Hakuna kitu kibaya kama mtu ambaye amehudumia Wakenya, amefanya kazi na anapoenda nyumba anaenda mikono mitupu. Mswahili anasema mikono mikavu hailambwi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}