GET /api/v0.1/hansard/entries/1499804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499804,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499804/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Baadhi ya wale madiwani ama councillors ambao wako Kirinyaga mpaka siku ya leo, baada ya Mswada uliopitishwa Bungeni ili walipwe pesa zao za uzeeni. Wengi wameaga dunia na shida nyingi za kiafya. Hawakuweza kujikimu ama kujitunza kwa sababu hawakulipwa pesa zao za uzeeni. Hata kama tunasukuma walipwe pesa zao, leo hii nasimama hapa kusema kuwa wazo hili ni nzuri kuhakikisha kwamba viongozi wetu baada ya kustaafu ama kukamilisha vipindi vyao vya huduma kwa wananchi hawapitii shida ambazo wengi wanapitia. Bw. Spika wa Muda, leo hii mimi kama Seneta nahudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Nikibahatika kurudi katika Bunge hili, nitakuwa nimehudumu kwa miaka 10. Hiyo inamaanisha kuwa nitakuwa napata pensheni kwa miaka ambayo nitaishi. Kuna pesa ambazo zinakatwa kwa mshahara wangu. Nikihudumu kwa kipindi cha miaka mitato, nitapewa gratuity wakati naenda nyumbani. Mfumo wa kuhakikisha kuwa watu wanapata pensheni au pesa za uzeeni ni mzuri zaidi. Kumekuwa na masikitiko makubwa. Tumekuwa tukichangia waliokuwa madiwani. Kuna mwingine ambaye alikuwa ameajiriwa kama mfanyikazi wa nyumbani ilhali alikuwa kiongozi aliyekuwa anahudumia wananchi. Mswada huu unapendekeza kuundwa kwa bodi ambayo itaangalia maslahi yao kwa kutenga pesa za uzeeni. Wengi wa watakaowekwa pale watakuwa wawakilishi wa wadi ambao wataweza kufanya uamuzi utakaowapa faida wenzao. Ni nadra sana kupata mtu ambaye aliwania kiti cha useneta kwenda kuwania uwakilishi wa wadi. Shida wanazokumbana nazo waliomaliza hatamu ya uongozi zitatatuliwa na Mswada ulio mbele yetu. Bw. Spika wa Muda, kuna jumbe fupi tunazopata kutoka kwa MCA s katika maeneo tofauti ya kaunti ambazo ni muhimu. Mwakilishi wa wadi anajua kila mtu. Kazi wanayofanya inaweza kufananishwa na ile ya machifu. Kukiwa na harambee kwa ajili ya ugonjwa au nyumba kuchomeka, wao ndio wa kwanza kualikwa. Wengi hutumia magari yao kama ambulensi kukiwa na wagonjwa. Najua tunaangalia maslahi yao kwa mambo ya pesa za uzeeni. Tunapozingatia maslahi yao, ni vizuri pia kuangazia Ward Fund ambayo walifaa kupewa. Wengi wanaoishia kuwa maskini ni wale ambao wanatumia pesa zao kusaidia wengine. Kwa nini wanasaidia na kuna pesa ya afya ambayo imetengwa? Hivi karibuni tutapitisha sheria ya kuhakikisha pesa zinaenda kwenye kaunti zetu ili kuhakikisha kuna dawa katika hospitali na barabara na shule za chekechea zinajengwa. Pesa wanazotoa wawakilishi wa wadi kila siku ni kuwezesha huduma kupatikana. Kwa hivyo, naunga mkono. Nawaambia MCAs wote katika nchi hii kwamba sisi kama Seneti tunawajali. Hii ni dalili kuwa tunawajali na tutaendelea kuwajali vivyo hivyo. Wao pia wanafaa kuchunga rasilmali katika kaunti zetu ili kusiwe na wizi ndiposa huduma ziwafikie wananchi. Hiyo itahakikisha kuwa fedha tunazopitisha hapa zinamfikia mwananchi. Kwa hayo mengi, Bw. Spika wa Muda, naunga mkono kuwa tuwe na bodi maalum ya kushughulikia pesa za uzeeni ambazo MCA"
}