GET /api/v0.1/hansard/entries/1499905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499905,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499905/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ninamshukuru Bi. Waziri pia kwa kujibu yale maswali nimeuliza, lakini niko na maswali mengine mawili. Kirinyaga upande wa Mwea, watu wameishi huko bila hati miliki kwa miaka na mikaka. Nyanyangu nilimzika akiwa na miaka 115 na bado hakuwa na hati miliki kwa sababu ya sheria gandamizi ya kunyunyizia mashamba maji. Swali langu la kwanza, ni juhudi zipi ziko kuhakikisha kwamba wakaazi wa sehemu za Mwera Irrigation Scheme na South Ngariama wamepata hati miliki na ni lini? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}