GET /api/v0.1/hansard/entries/1499926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499926,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499926/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza kabisa Bi. Waziri, ninakupa heko kwa kuweka sahihi kwa mkataba wa kutaka kuendelea na kazi yako ya uwaziri hapo jana. Kama unavyojua, Kaunti ya Kilifi ambapo mimi ni Seneta, ni eneo la pwani ambalo linajulikana sana kwa mambo ya maskwota katika Kenya nzima. Ninafikiria hakuna kaunti ambayo ina maskwota wengi zaidi ya Kaunti ya Kilifi. Nikizingatia ya kwamba tunaweza kulingalisa na sasa hivi ambapo kumekuwa na wingi wa watu ambao wanataka kujenga majumba na watu ambao wamekuja kuweka raslimali zao na kutafuta vile wanaweza kujiendeleza kimaisha na kibiashara. Hilo ni jambo nzuri. Hata hivyo, tukiangalia zaidi, tunaona ya kwamba kumekuwa na hali ngumu ya maskwota. Maskwota wanaendelea kugandamizwa. Wanawekwa katika meneo ya kando ambayo sio maeneo ambapo wanaishi. Sio kilifi tu, eneo Bunge la Ganze, Magarini, Malindi na hata Eneo Bunge la Kilifi South, kumekuwa na muamko mkubwa. Ukiangalia katika eneo la Vipingo, Kikampala na Mtwapa, kumekuwa na maskwota wengi sana na sasa wanasongeshwa na kupelekwa katika hali ya kuishi kana kwamba wao sio binadamu tena."
}