GET /api/v0.1/hansard/entries/1499929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499929,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499929/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, watu wanajenga majumba na wengine kuyanunua na wakija pale huwa wanakuja na hati miliki wakisema ya kwamba wao ndio wamiliki. Watu wengine wanavurushwa kwa kutumia polisi. Polisi wanatumiwa vibaya kwa kuambiwa endeni mukawaondoe watu katika makao yao. Je, ni hatua gani ambayo Wizara yako ambayo inahusika na utetezi kama huu, unaweza kutetea maskwota ama ni hatua gani Wizara yako inachukua kuona ya kwamba maskwota wanoishi kama ni Kaloleni, Rabai--- Ukiangali Eneo Bunge la Rabai, sasa hivi lote limevamiwa na waegezaji wanotaka kuja na kuweka mali zao na kila kitu. Wameichukua ardhi ile na kusongesha wenyeji waliozaliwa pale. Mahali pale kuna makaburi, makanisa, misikiti na pia sikuli. Sasa wamekuja na orders, wakiwa na buldozers za kuangusha nyumba na kuvurusha watu. Wizara yako ni muhimu sana. Je, ni hatua gani ambayo Wizara yako imechukua kuwatetea maskwotai? Sisi hatukatai maendeleo, lakini vile vile, wakaaji waliozaliwa pale na wanaoishi pale, hatalazimishwa kuondoka pale. Pia pale pana makaburi yao. Kwa hiyo, siyo vizuri kupeleka tingatinga pale na kubomoa nyumba za watu na wengine wanaweza kuwa na title deeds."
}