GET /api/v0.1/hansard/entries/1502002/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502002,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502002/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kuniruhusu nichangie Hoja ya Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kenya iliyokuwa siku ya Alhamisi katika Bunge La Taifa. Shughuli hii iliwaleta pamoja Maseneta na Wajumbe wa Bunge la Taifa. Naunga mkono Hotuba ya Rais kwa sababu iligusia masuala ya kilimo ambapo mimi ndiye naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Alizungumzia suala hili kwa urefu. Nakumbuka vyema Serikali ya Kenya Kwanza iliposhika hatamu, mbolea ilikuwa inauzwa Shilingi 6,500 za Kenya. Wakati huu wa kipindi cha miaka miwili, mbolea hii hii sasa inauzwa shilingi 2,500 za Kenya ili mwananchi awe na pesa mfukoni. Masuala ya kilimo ni njia moja ya kuchangia uchumi wa Kenya. Wakulima wengi wanaofanya ukulima wa kahawa, majani chai, makadamia, miraa, muguka, pamba, miwa katika sehemu za Bonde la Ufa na maembe, wote wanahitaji mbolea. Inafaa kaunti zote 47 zijengewe mabwawa ili kilimo kiweze kundelea vilivyo. Niko na imani Rais atatimiza. Tunapendekeza bei ya maziwa iwe shilingi hamsini na wakulima husika walipwe kwa kipindi cha mwezi mmoja. Biblia husema, mko na macho na hamuoni, na mko na masikio wala hamsikii. Tukiangalia majani chai, kila mtu anasheherekea kwa sababu kilimo hiki kinaleta faida ambayo haijashudiwa kwa vipindi vya awali. Vile vile, bei ya kahawa imeenda juu. Vile vile Rais alipendekeza kilimo kiwe cha kuongeza dhamana ili mambo yote ya ukulima yarudi mashinani kwa kaunti zetu zote kama inavyotakikana kwa mfumo huu wa ugatuzi. Ningeomba Seneti tumuunge mkono Rais kwa kipindi hiki. Aidha, Rais alizungumzia masuala ya waalimu. Ukilinganisha kipindi cha awamu cha Rais Mstaafu na awamu hii ya Rais aliye mamlakani, kwa muda wa miaka miwili, Serikali ya Kenya Kwanza imeajiri waalimu 56,000 na ameahidi kuongozea wengine. Hivyo basi, naomba tumuunge mkono kwa azma yake ya kuboresha elimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}