GET /api/v0.1/hansard/entries/1502003/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502003,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502003/?format=api",
"text_counter": 205,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ni kweli kuna shida ya shule za vyuo vikuu na inafaa iangaliwe. Pia, Serikali haina wafanyikazi wa kwenda mashinani kuhamasisha watu kuhusu miradi ya Serikali ambayo Rais amekuwa akizindua mara kwa mara. Rais pia alizungumzia suala na halmashauri ya Social Health Authority (SHA) ambayo inasimamia Bima ya Afya ya Jamii almaarufu Social Health Insurance Fund (SHIF). Ombi langu ni tuiunge mkono Serikali ya Kenya Kwanza. Sisi wafanyikazi wote tunateseka na kuumia kwa kutozwa pesa. Baadhi yetu tunatozwa shilingi 20,000 na hata wengine 30,000. Hata hivyo, tunaelezwa kuwa itakapoanza kufanya sawasawa, watu wote wanaougua saratani na magonjwa mengine kama vile kifua kikuu yatashughulikiwa. Magonjwa hayo yametusumbua sana kama Wajumbe kwa kufanya michango ya kila mara kule mashinani itaisha. Mpango huu ukifaulu wagonjwa hao wote hawatakuwa walikipa pesa. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu naomba niongezee kwa kusema hivi. Serikali ya hayati Rais Kibaki ilisema kuwa kila mtu akifisha miaka sabini awe akipata msaada wa pesa fulani. Serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta haikuongezea idadi ya walengwa. Katika Serikali ya Kenya Kwanza mtu mwenye miaka sabini na kuendelea anapata pesa kila mwezi. Kama tukimshikilia rais, tunaona Serikali yake inaendelea kwa njia inayofaa. Wanaofanya kazi ya Community Health Promoters kule vijijini wanalipwa shilingi 5,000. Hata hivyo kuna matatizo kwa sababu Wabunge wa Bunge la Kitaifa wanakataa kuidhinisha pesa kwa kaunti. Nawarai Wajumbe wa Mbunge la Taifa watuongezee zile pesa ili Community Health Promoters walioajiriwa na Serikali ya Kenya Kwanza waweze kupata mishahara. Rais pia aliguzia suala la Adani Group. Naomba niwajuze Seneta wa Nairobi, Sen. Maanzo wa Kaunti ya Makueni na Seneta wa Kitui ambaye ni Bishop kwamba tuunge mkono Serikali ya Kenya Kwanza ili ifanye kazi inayofaa. Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Siku ya Hotuba, Rais pia alifutilia mbali kandarasi ya Uwanja Wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na ile ya Kampuni ya Usambazaji Umeme Nchini (KeTRACO). Pia aliahidi mambo uya procurement yatakuwa katika mtambo wa e-Citizen. Hivyo basi, sio lazima kila siku tuwe ni kupigana hapa na pale. Naomba tuiunge mkono Serikali kwani hata hali ya uchumi imeimarika. Rais aliambia Taifa ya kwamba, alipochukua hatamu mambo ya i nflation illikuwa nine per cent na sasa ni 2.7 per cent. Tuugangeni pamoja kwani umoja ni nguvu. Serikali hii iko na maono angalau tuone tutamiliza muhula huu vipi. Sio kila wakati ni kupiga Serikali. Kwa suala la Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), nakumbuka mwaka jana kama Serikali ya Kenya Kwanza tulipitisha majina saba. Baadaye, ikasemekana lazima upande wa Mrengo wa Walio Wachache Bungeni wa Azimio na wengine sharti waongezee watu wawili. Hii ndiyo imeleta shida. Kwa hivyo, naomba Maseneta wote tuungane pamoja ili tushikilie serikali ya Kenya Kwanza. Tukifanya hivyo, mapato ya Serikali ya Kitaifa na yale ya kaunti 47 yataimarika. Bw. Spika wa Muda, ni mimi Seneta wa Kaunti ya Embu, Daktari Alexander Munyi Mundigi. Naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}