GET /api/v0.1/hansard/entries/1502004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502004,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502004/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais ya Hali Halisi ya Taifa iliyotolewa mnano tarehe 21.11.2024 kuambatana na Kifungu Cha 132(1) ( C) cha Katiba yetu. Ninampongeza Rais kwa kutekeleza jukumu hili la kikatiba ambalo ni muhimu sana la kujuza Bunge kwa mujibu wa Katiba. Bw. Spika wa Muda, ni masikitiko kwamba katika Hotuba yake, Rais hakuzungumzia maswala ya ugatuzi. Hotuba yake yote haikugusia maswala ya serikali za kaunti ambazo ni kiungo muhimu katika nchi yetu. Ikumbukwe kwamba tulikuwa na mvutano kuhusu Division of Revenue Bill ambapo mpaka wiki iliyopita ndipo Kamati ya Uwiano iliweza kukubaliana kuhusu kiwango cha pesa zitakazokwenda kwa kaunti zetu. Tangu mwezi wa saba hadi wa kumi mwaka huu, kiwango cha fedha za kaunti kilikuwa hakijulikani. Kwa hivyo, kulikuwa na shida ya kaunti zetu kupata pesa kutoka kwa Hazina Kuu ya Kitaifa. Ijapokuwa sheria inatoa fursa kwa Hazina Kuu ya Kitaifa kulipa mpaka nusu ya pesa ambazo zilipelekwa katika kaunti zetu mwaka uliotangulia, Serikali imekuwa na shida ya kutuma pesa, hivyo basi kuziweka serikali za magatuzi katika nchi yetu katika hali ngumu ya kulipa madeni na kulipia huduma ambazo wanatoa katika kaunti tofauti tofauti. Pesa zilitumwa katika kaunti zetu wiki mbili zilizopita. Hata hivyo, kaunti nyingi zimepata hasara kwa sababu ilibidi wakope pesa kwa riba ya juu ili walipe mishahara na huduma nyingine. Jambo la pili ambalo limenisikitisha ni hali ya haki za binadamu katika nchi yetu. Wakati wa maandamano ya Gen Z, vijana wengi walipigwa risasi na kuuawa kiholela. Ijapokuwa Rais alitoa hakikisho kwamba wale wote ambao waliua bila hatia watachukuliwa hatua, mpaka sasa, hatujaona jambo lolote ambalo limefanyika kutekeleza matamshi hayo ya Rais na vile vile kuhakikishia familia za wale ambao waliondoka kwamba haki itatendendeka kuhusiana na watoto na jamaa wao. Jambo lingine la kusikitisha pia ni kwamba maswala ya utekajinyara yamezidi katika nchi yetu. Cha hivi karibuni ni kisa ambacho watu wanne wa asili ya Kituruki walitekwa nyara hapa Nairobi na kupelekwa Turkey bila familia zao kujulishwa wala sheria kufuatwa. Sheria yetu inasema kuwa iwapo mhalifu yuko hapa na anatakikana katika nchi nyingine na kuna makubaliano kati ya nchi yetu na nchi anayotakikana kupelekwa kortini, anafaa kufanyiwa kesi ya uhamisho kabla ya kwenda kushtakiwa kuhusu makosa aliyofanya kule. Licha ya kuwa na sheria, watu wale walirejeshwa Istanbul kule Uturuki ili kushtakiwa kwa makosa ambayo hayajulikani. Ikumbukwe kuwa walikuwa wahamiaji halali katika nchi yetu ya Kenya. Ina maana kwamba mhamiaji yeyote hayuko salama katika nchi aliyohamia. Mwingine aliyechukuliwa wiki mbili zilizopita ni Kiongozi wa Upinzani kule Uganda, (Dr.) Kizza Besigye. Alichukuliwa hapa Nairobi katika hali hiyo. Utekajinyara na mauaji ya kiholela, ama extrajudicial killings, ni mambo ambayo Rais alifaa kuzungumzia kwa undani zaidi kwa sababu ni mambo ambayo yanahusiana na usalama wa Wakenya. Hata mimi binafsi sina usalama kwa sababu watu wanatekwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}