GET /api/v0.1/hansard/entries/1502005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502005/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "nyara na mwishowe kupatikana wameuawa. Wengi wa waliouawa ni vijana ambao walishiriki katika maandamano ya Gen Z. Vile vile, tulitarajia Rais kuzungumzia tuhuma ambazo Gen Z walikuwa nazo wakati walipokuwa wanaandamana hadi kwenye Bunge hili mwezi wa sita mwaka huu. Hata hivyo, Rais hakugusia hayo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba Rais pamoja na washauri wake hawasikii wala kufuata mambo mengi ambayo yanaathiri Wakenya. Ijapokuwa Kenya yetu ni democrasia, maswala ya mauaji ya kiholela, utekajinyara, na ukandamizaji wa haki za kibinadamu kupitia mambo kama vile mauji na mengineyo yanatia doa nchi yetu kwa sababu Kenya ni mwanachama wa Community ofNations . Tumetia sahihi kwenye mikataba mingi kuhusu kuwalinda wahamiaji na haki za kibinadamu. Tumetia sahihi mikataba mingine mingi ambayo hatuwezi kupuuza kwa sababu sisi tumekubalika katika Community of Nations . Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, Hotuba hiyo haikukamilika kwa sababu mambo ambayo tumezungumzia ni muhimu na yalifaa kuangaziwa na Rais katika Hotuba yake."
}