GET /api/v0.1/hansard/entries/1502011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502011/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante sana Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nampa kongole Rais kwa kutoa Hotuba yake ya hali halisi ya nchi ya Kenya ya mwaka huu. Sikudhani angefanya hivyo kwa sababu siku zilikuwa zimeyoyoma na mwaka unaenda kuisha. Kalenda ya Bunge ilikuwa imefika mwisho, kwani tumebaki na siku saba ili Bunge liende kwa likizo. Lakini ni vyema alikuja kutoa Hotuba ya hali halisi ya Taifa ya mwaka wa 2024. Kitu cha muhimu katika Hotuba ya Rais ni kugusia mambo mbalimbali ya muhimu ambayo wananchi wa Kenya wangependa kusikia na kuona suluhisho limepatikana. Bw. Spika wa Muda, katika Hotuba ambayo Rais alitoa, hakuweza kugusia kitu cha muhimu kilichotendeka mwaka huu katika maeneo yetu ya Bunge, ilhali alitoa Hotuba hiyo akiwa Bunge. Kitendo cha muhimu kilichotendeka Bungeni ni kuuawa kwa vijana wa kike na kiume katika barabara tofauti hapa Nairobi. Wengi walipoteza maisha yao katika maeneo ya Bunge. Kwa hivyo, ilikuwa ni muhimu kwa Raisi kutaja mambo hayo akitoa Hotuba yake ya 2024 akiwa ndani ya Bunge, mahali ambapo vijana wadogo; Generation Z, walipigwa risasi na polisi wetu na wakafa. Hatuwezi kusema ni wangapi, lakini waliokufa na kupata majeraha na walio hospitalini hadi sasa ni wengi. Kuna wengi waliokufa na hawakupatikana na wazazi wao bado wanawatafuta, kwani hawajui waliko. Ilikuwa ni muhimu aeleze Wakenya kinaga ubaga katika Hotuba yake watoto waliopotea wako wapi. Je, waliopata majeraha wamepata matibabu? Je, gharama ya waliopata majeraha na kuenda hospitali kutibiwa zimelipwa? Je, Serikali imechukua hatua gani kwa waliopoteza maisha yao, ikiwa Bunge limepitisha Hoja ya kwamba waliopoteza maisha na walioumia walipwe kulingana na maumivu yao au hela waliotumia kuzika wapendwa wao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}