GET /api/v0.1/hansard/entries/1502012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502012,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502012/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Pili ni kwamba, ilikuwa ni muhimu aweze kukemea ama aseme katika Hotuba yake kwamba, hakufurahia vitendo vilivyofanywa na polisi walipotumia nguvu zaidi kuliko walivyokuwa wamefunzwa kule Kiganjo, jinsi ya kupambana na kesi kama hiyo. Hawa walikuwa vijana wadogo, waliruka ukuta na kuenda dining room, wakakula chakula kilichokuwa pale. Wengine waliingia ndani ya Bunge na kusema waliyoyasema. Lakini kuna watoto wetu ambao waliumia. Bw. Spika wa Muda, sasa watu wamesonga mbele. Wale walioumia wakati wa mgomo, natumai kwamba Rais atatafakari na atachukua hatua ya kuona ya kwamba hao vijana wa Gen-Z watapata afueni katika hospitali; na kama kulikuwa na mazishi, pesa zao zilipwe na wale waliopata ajali, wapatiwe huduma. Pia ningependa tuzingatie kwamba elimu ndio msingi wa maendeleo. Mambo ya elimu yalikuwa muhimu sana katika Hotuba hii; hususan anafaa atueleze kwa nini hivi sasa katika historia ya Kenya tangu tupate Uhuru, kumekuwa na migomo nyingi katika kila sekta. Ya muhimu zaidi ni kwamba kumekuwa na migomo za walimu kuanzia university, Kenya National Union of Post Primary Education Teachers (KUPPET) na Kenya National Union of Teachers (KNUT). Jambo gani linazusha migomo hii? Hilo ni jambo muhimu ambalo angezingatia katika Hotuba yake ya mwaka huu. Angetueleza ni hatua gani Serikali inachukua kusuluhisha swala la migomo ya walimu ambayo inatendeka kila uchao. Hivi sasa tunapoongea maprofesa wa chuo cha Moi, University of Nairobi, na kwingine wamegoma. Ingekuwa muhimu zaidi kuona Rais akiweka swala hili katika Taarifa yake ambayo alihutubia Wakenya, mwaka huu. Lakini, hakuweka. Migomo hiyo inaendelea mpaka sasa na hajaweza kutupatia suluhu. Hili lilikuwa jukumu lake muhimu kuwaambia Wakenya ili watoto wetu ambao tunawapeleka university waweze kumaliza masomo yao wakati unaohitajika na sio kuketi kule na kumaliza course ya miaka minne kwa miaka sita. Hii haitakuwa jambo la heshima au jambo nzuri. Nataka kugusia swala la uchumi wa nchi yetu ya Kenya. Kwa sasa tunaona ya kwamba kuna afueni kidogo, lakini hii haijatosha. Afueni kidogo imeingia na tunaona bei ya vitu vidogo kama unga imerudi chini na pia mboga zinapatikana. Lakini mambo mengi ya kuweza kuchukua mkono, kuweka kwenye sahani na kuchukua chakula na kula, bado yako na shida. Mambo mengi bado ni magumu. Ingekuwa muhimu kama Rais angeweza kuangalia haya mambo. Bw. Spika wa Muda, tuko na mambo ya medical insurance covers; kuna SHA na SHIF. Rais angechukua nafasi ili kufafanua jambo hili. Hatuoni hizi insurance zote mbili zikifanya kazi kikamilifu. Wengi wamekwenda kupata matibabu katika mahospitali na wakaambiwa hawawezi kutibiwa kutumia hizo insurance. Mimi mwenyewa nilienda kumwona daktari wangu na nikamuuliza kwa nini sioni watu hapo wakitumia kadi zao za SHIF na SHA. Akasema hizo hawakubaliani nazo. Ilkiwa madaktari wenyewe wale professionals hawakubaliani na hizo, hii inamaanisha kwamba bado kuna shida. Rais anaweza kuwa na nia nzuri ya kuona ya kwamba kila mtu anapata huduma za kujifaidisha kiafya lakini ikifika wakati wa implementation wengi wanambwaga Rais. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}