GET /api/v0.1/hansard/entries/1502013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502013,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502013/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Inaweza kuwa sio makosa yake. Yeye anafikiria kwamba watu wana implement, lakini watu wengine wanamchelewesha katika tegemeo lake la kuwasaidia Wakenya. Hivi sasa, hizo medical covers za SHIF na SHA, zote ziko na shida ama hazifanyi kazi. Bw. Spika wa Muda, vile vile, mawaziri wake wanafaa kutimiza yale anayoyasema Rais. Lakini mara nyingi tunaona jambo la kusikitisha ambapo Rais anaelekeza kitu lakini jambo hili linakosa kutekelezwa. Wale basi, wanambwaga Rais. Kuna haja gani Rais aseme kwamba kutakuwa na Collective Bargaining Agreement (CBA) na inafaa kutiwa kidole na Waziri wa Elimu ama Waziri wa Afya; ambaye anafaa kutekeleza mishahara fulani baada ya miaka miwili alafu asitekeleze jukumu hilo? Hii ndio inaleta mambo ya migomo. Ingekuwa bora Rais awaambie watu wake kwamba: Kutoka wakati huu sitaki Waziri wangu atie sahihi CBA ya wafanyikazi bila kuona hali ya uchumi au kuona kwamba Serikali itatimiza wajibu wake wa kukamilisha deni la walimu au watekelezaji kazi katika pande zote zinazotakikana kama afya na zinginezo. Bw. Spika wa Muda, Rais katika Hotuba yake aliongea vizuri kuhusu---"
}