GET /api/v0.1/hansard/entries/1502017/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502017,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502017/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " I want to touch on important aspects. Jambo la kwanza ni kuwa, Rais aligusia mambo mengi mazuri. Aliongea kuhusu sukari, mahindi, kahawa, na majani chai. Kimaendeleo, zitasaidia namna gani? Kati ya mimea aliyozungumzia, kuna mimea miwili muhimu sana kutoka sehemu ninayotoka. Upande wa Kilifi kunakuzwa korosho na mananasi. Mkorosho ni mmea muhimu sana kwa maisha ya wakulima kule, pamoja na mananasi. Vitu vingi vinaweza kupatikana kwa urahisi kwa sababu ile ardhi inakuza mmea kama mkorosho. Ingekuwa vyema kama Rais angezungumzia hatua ambazo Serikali imechukuwa kutenga pesa zitakazopewa wakulima hawa wanaopanda na kuuza korosho, mananasi na maembe, kwa sababu hawa pia ni wanabiashara kule. Hivi sasa tunajipata katika hali ya uchochole kule Kilifi. Kulikuwa na maendeleo sana lakini hivi sasa hakuna kazi, na vijana hawa wameketi tu. Watu hawa wanaishia kukula muguka na kutenda maovu. Ikiwa Rais anapanga chochote hivi sasa, anafaa kutabaini kuwa mkorosho ndani ya Kaunti ya Kilifi unaweza kuwasaidia watu wengi kwa kupata mapato ya kazi. Mwisho, nampa kongole Rais kuhusu mambo ya Adani. Huyu ni mtu ambaye pengine angezorotesha nchi yetu katika hali ya uchumi. Lakini aliona mbele na kuamua kuwa ni bora kuwaambia Wakenya kuwa hiyo njia haifai. Zaidi ni kuwa, tuliona President Trump mwenyewe akikataa hizo deal za Adani. Serikali ya Amerika pia ikasema kuwa ashikwe na hatimaye hakumaliza siku 24. Sio kama sisi ambao tukielekeza mtu fulani ashikwe anaweza kupotea kwa wiki nzima. Kule Amerika maagizo yalipita kuwa Adani ashikwe kabla ya masaa 24. Hatua ambayo Rais alichukuwa ilikuwa safi. Hii ni pamoja na hatua ya Kenya Electricity The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}