GET /api/v0.1/hansard/entries/1502024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502024/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Basi nitataja tu na niseme ya kwamba, kuna Mswada muhimu sana ambao tumekuwa tukiuzunguka kama Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uchumi wa Baharini katika Seneti. Tushaenda Kwale mpaka Lamu, na ninadhani tutakapo malizana na ule Mswada itakuwa ni rahisi sana kuhakikisha ya kwamba korosho, macadamia, ufuta, nazi na vitu kama hizo zinatiliwa maanani. Hii ni kwa sababu, sheria ambayo iko kwa sasa, inafaa kufuatiliwa. Ujuavyo, wakati Mswada huu utakuja katika Bunge la Seneti, tutauunga mkono. Kwanza ningetaka niongee mambo mawili ama matatu. Kwanza ni kwamba, Katiba yetu inaruhusu Rais kuja kutoa Taarifa katika Bunge la Kitaifa. Ni vizuri anakuja kueleza mambo yanayoendelea; yawe mazuri ama mabaya. Nampa kongole kwa sababu, Mswahili husema; mrina haogopi nyuki. Kwa hivyo, mambo yawe mazuri ama mabaya, lazima yasemwe ili Wakenya waweze kuyajua. Nitaongea kidogo kuhusu kilimo na nitakuwa nikikahiri wakili kama sitasema kwamba mbolea ya ruzuku ambayo Serikali imekuwa ikipeana imewasaidia pakubwa wakulima. Mwanzo ilianzia vizuri na imeendelea, lakini zile taasisi na nyenzo za Serikali ambazo zinafanya kazi katika Wizara ya Ukulima, lazima zitie bidii, sana sana waweze kuangalia kile kilimo ambacho kinafanyika. Hii ni kwa sababu chakula kingi ambacho kinatayarishwa huwa kinafanywa kwa misimu. Bw. Spika wa Muda, kama leo nimepokea simu fifi, kwa kimombo; missed call, kutoka kwa wakulima katika eneo la Mwea, ambao wanasema ni kweli mbolea ya kupanda pamoja na mbolea inavyowekwa wakati mimea inaendelea kukua iko. Hata hivyo, zile sheria ambazo ziko pale ni kwamba wakati huu wanavuna na wanastahili kuchukua mbolea za kupanda. Lakini wanaambiwa mikakati yenye iko, lazima kwanza wachukue mbolea ambayo inawekwa kwa mmea ukiwa unaendelea kukua. Lazima wachukue hiyo mbolea kwa sababu hawajafungua ile mbolea inawekwa kwa mchele wakati unapandwa. Madini ambayo yanatakikana na mmea wakati unapandwa ni tofauti na ile ambayo inatumika wakati mmea ni mkubwa. Kwa hivyo, ningeuliza wizara ya ukulima The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}