GET /api/v0.1/hansard/entries/1502025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502025,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502025/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "iweze kufungua kwa sababu mbolea isha nunuliwa na iko pale, iweze kupewa mkulima. Hii ni kwa sababu ikiwekwa pale, itakuwa haina maana. Ujuavyo, changirizi ya chungu huua hata ndovu. Shida tulizo nazo ndogo ndogo zile za mkulima ambaye amecheleweshwa kupewa mbolea ambayo serikali ishanunua na kupeleka mahali pale, ndio inasababisha yule mkulima kujiandaa na kutoa chakula ambayo inatosha, anarudi nyuma. Kwa hivyo, kama wale ambao wako katika taasisi husika yaani Cereals Produce Board (CPB), kama wangeweza kulainisha ili wakulima wapate voucher na mtu apewa mbolea ambayo wanahitaji, ingekuwa vyema zaidi. Kwa sababu, unapoenda pale unapata yule mtu ambaye anataka mifuko kumi, ananyimwa na kupewa mfuko mmoja, lakini mbolea bado iko pale. Wale wanaofika mapema waweze kupewa mbolea ili waende wakalime. Nitaguzia pia kuhusu kuuliwa kwa wanawake kwa sababu imezidi sana. Hili si jambo la kawaida, kwa sababu kawaida mwanaume vile ameumbwa si wa kupiga ama kuumiza wanawake. Rais amesema kwamba, yeye mwenyewe, hataruhusu mambo hayo kuendelea. Sasa kuna Wizara ya Usalama, Directorate of Criminal Investigations (DCI) na polisi. Kazi kwao ili waweze kutafuta wale wanaume ambao wanafanya mambo ambayo hayafai. Tunapoendelea hivi, kuna siku kumi na sita za wanaharakati kuhakikisha ya kwamba mauaji ya wanawake inapungua ama imemalizwa kabisa. Lakini, wakati ambao unaotumiwa kwa mwanamke anapoumizwa na kushikwa, nadhani bado tunafaa tuangalie zaidi. Tuweze pia kuhakikisha kwamba wanaopelekwa wanafungwa kabisa kuhakikisha kwamba wale ambao wana tabia kama hizo hawazirudia. Ukulima ni jambo la maana sana. Ukweli ni kwamba bei ya kahawa inaendelea kupanda. Leo nilikuwa nikiangalia bei ya kahawa katika soko la kimataifa na ni kweli imeendelea kupanda. Pia kuna pesa ambayo inapeanwa kwa wakulima ambayo inaitwa Cherry Fund na kuna pesa ingine inaitwa Commodities Fund, ambayo iko na imewekwa na Serikali. Hata hivyo, Kenya Planters Cooperative Union (KPCU) inafaa itafute njia ya kupata ile fedha iwe rahisi kwa mkulima wa kawaida kama nyanya anaye lima kahawa. Isiwe ni jambo msaragambo ya mtu yeyote ambaye anataka kuchukua zile fedha, ili waweze kuzichukua kwa wingi na tuongeza ukulima wa kahawa na vile vile kuweza kununua miche na kupeana. Kwa sababu unajua kwamba, ukulima pia umegatuliwa. Juzi nilikuwa naangalia katika runinga nikaona gavana wa Makueni akipeana miche ya kahawa na kusema kwamba anajaribu kuhakisha ya kwamba, mazao ya kahawa inaongezeka katika gatuzi la Makueni. Basi mimi ningeuliza magavana, kwa sababu ukulima umegatuliwa, pia waende wapambane na wahakikishe kwamba wakulima wanapata miche aina tofauti tofauti. Kama ni mikorocho au parachichi ipeanwe, ili wakulima waweze kufaidika. Bw. Spika wa Muda, afichaye mgonjwa hufichuliwa bila kilio. Nimesikia wengi wakiongea na mimi nitaongea juu ya mambo ya Adani. Serikali ishaona ya kwamba Adani si mtu ambaye anaweza kufanya kazi hapa. Nadhani hivyo ndivyo inavyofaa. Hii ni kwa sababu jambo likionekana likiongelewa sana, wakati limeongelewa na Rais, nadhani watu wanaichukulia kwa uzito. Nadhani hilo ni jambo nzuri kuwa akae kando ili The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}