GET /api/v0.1/hansard/entries/1502028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502028,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502028/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "pale Sagana. Kwa muda mrefu sana imefikisha hadhi ya kupewa JuniorSecondary ambayo kwa sasa wamekuwa cleared . Nilikuwa nimetuma barua hata kwa waziri na kwa sababu mambo ambayo inasemwa, mwenye kuenda pale kufanya kazi ya mkono ni hao mawaziri na makatibu katika zile wizara. Pia ni vizuri waangalie na kuhakisha ya kwamba zile shule zinahitaji kupandishwa hadhi zipandishwe ili watoto wasikuwe wakienda safari ndefu sana kuenda kutafuta Elimu. Nikimalizia, nitasema kwamba mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uchumi wa Baharini katika kamati ya Seneti, mkulima ni mtu wa maana sana. Tunahitaji mkulima asubuhi tunapotafuta staftahi. Saa nne wakati unapokunywa chai ambayo iko na maziwa na majani pia. Saa saba katika chakula cha mchana na cha jioni. Tunamuhitaji mkulima zaidi ya mara tano kwa siku kushinda mtu yeyote yule mwingine. Kwa hivyo, kufuatilia ile bidii imeekwa kuhakisha kwamba mkulima anafaidika, tuendelee kuwasikiliza wakulima. Ni kweli walituchagua na unajua chemichemi si mtemi, ukitaka maji mpaka uiname. Hiyo ni kusema hata wakulima wanakaa wadogo wadogo lakini ni wadosi wetu. Tuwasikize na tunaendelea kuwasikiliza, kuhakikisha kwamba wamepata kila kitu wanayohitaji ili tuweze kuzalisha chakula ya kutosha katika nchi hii na wao waendelee kuimarika. Asante sana."
}