GET /api/v0.1/hansard/entries/1502298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502298,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502298/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa ili nichangie Hotuba ya Mheshimiwa Rais. Ninampongeza Rais pia ninamwunga mkono kwa yale aliyoyasema. Mombasa tunasema aliitoa hiyo Hotuba kichwa kikavu, yaani, bila kusoma mahali. Kwa hivyo, alijua kile alichosema. Aligusia mambo kadha wa kadha ikiwemo mambo ya usalama. Hatuwezi tukafanya mambo ya maendeleo bila usalama. Vile vile, ninamwunga mkono haswa kwa sababu nilichukua hatamu ya uongozi Lamu tukiwa tunahudumiwa na Kituo cha Polisi cha Changamwe. Hiki kituo kilisimamia Jomvu na Changamwe. Jambo hili lina umuhimu sana na hii leo, tumelitia maanani sana katika wadi ninazoziwakilisha. Kwa sasa, kila wadi iko na kituo cha polisi kinachoisimamia."
}