GET /api/v0.1/hansard/entries/1502299/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502299,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502299/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Mheshimiwa Rais alizungumzia mambo ya huduma ya matibabu. Ninawasihi watu wa maeneo yetu, haswa Jomvu, waendelee na usajili wa mambo ya huduma ya matibabu kwa sababu tunataka watu wetu wapate huduma vile Rais Ruto alivyosema. Alizungumzia pia mfumo wa elimu na tunaona mambo yanaendelea kuwa mazuri. Sisi kama viongozi wa Pwani tumekuwa na mkutano naye Rais pale Ikulu ya Nairobi na amezungumzia mambo ya elimu. Kuna umuhimu wa kuongeza waalimu vile alivyosema ili tusaidie watoto wetu wapate elimu. Hakuna siasa inayokosa maneno; watu wanapiga maneno sana. Leo hii, tumeona nyumba nyingi zimejengwa kule Buxton na sehemu nyingine. Katika lugha ya Kiingereza, tunaita nyumba hizo affordable housing . Watu wameanza kufaidika. Yule ambaye hataki kufaidika akae kando na awache wale ambao wanataka kufaidika. Makao ni jambo muhimu katika maisha ya binadamu. Nilipokwenda Homa Bay wakati fulani, nilisimama na Mheshimiwa Bensuda aliyekariri sana kuhusu kuhakikisha kuwa watu"
}