GET /api/v0.1/hansard/entries/1502341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502341,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502341/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Agnes Mantaine",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Narok North, JP) Asante sana Mhe Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ilinichangie Hotuba ya Mhe Rais katika Bunge hili. Nilisikiliza hiyo Hotuba kwa makini sana. Ningependa kumshukuru Rais kwa vile alizungumza na vile alivyoonyesha kwa makini alichokua akizungumzia. Ningependa kuanza na masuala ya elimu. Hakuna wakati ambao tumeweza kuajiri walimu wengi kama vile tumeajiri. Tumeajiri waalimu 46,000, na tutaajiri wengine 20,000. Hii si kusema kwamba wametosha, lakini ni kuonyesha nia yake kwa elimu ni nzuri. Ninampongeza kwa jambo hilo. Tulikuwa na shida nyingi kwa JSS. Sasa tumeona madarasa yameanza kujengwa. Pia, tukishapata waalimu na madarasa, basi tutakuwa na mwelekeo na tutaendelea kujua vile tutakavyoendelea."
}