GET /api/v0.1/hansard/entries/1502346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502346,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502346/?format=api",
    "text_counter": 263,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Agnes Mantaine",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa suala la uongozi wa hii nchi, hauwezi toshelesha kila mtu kisiasa. Kutakuwa tu na kelele. Ninampa heko Rais kwa kusimama kidete na kuzungumzia agenda yake vizuri na kuielezea kwa sababu ni lazima watu wataongea. Lakini ningependa kuomba Serikali ihakikishe wamama wana amani. Pia, ihakikishe barabara zimetengenezwa ili zitumike kuwapeleka wagonjwa hospitali. Pia, ninashukuru kwa sababu tutapata maafisa wa kuwasajili watu kwa SHIF. Tutaenda kuhakikisha wananchi wamejisajili ili waweze kupata matibabu na huduma. Hakuna namna tunaweza kusema hawatajisajili."
}