GET /api/v0.1/hansard/entries/1502458/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502458,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502458/?format=api",
"text_counter": 64,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "kusikiliza Hotuba ya Rais na vitu ambavyo amevifanya, hajavifanya kwa maneno pekee bali kwa vitendo ambavyo tumeviona. Kwanza, ningependa kumpongeza kwa kuwapatia vijana wa taifa hili ajira. Nimekuwa katika sekta ya ajira kwa miaka 25. Niliweza kuwasafirisha vijana 65,000 wakapata ajira nje. Mkondo huo ambao Rais ameuchukua pia unafuatiliwa katika mataifa ya Philippines, Indonesia na India. Wote wameshika ile market ya Middle East . Hizo siyo ajira za kazi za ndani pekee. Ametafuta ajira za madktari, nurses na engineers, yaani katika sekta tofauti tofauti. Nataka kumpongeza kwa kazi 103,000 ambazo amewapatia vijana wetu hivi karibuni. Nataka pia nimpongeze Rais kwa Taifa Care. Hiyo huduma ya afya itamsaidia mpaka yule mwananchi wa chini ambaye hana mshahara. Ameizindua huduma hiyo ili kumsaidia yule mama ambaye anauza maji, yule anayesukuma mkokoteni, na wale wanaoishi maisha duni, ili waweze kwenda hospitalini na kupata huduma. Ningependa kumpongeza pia kwa sababu kwa mara ya kwanza, hatujakuwa na njaa huku Kenya mwaka huu. Hiyo ni kwa sababu mwaka jana, Rais aliwekeza kwenye ukulima na tumeyaona matunda ya ukulima. Chakula kimejaa na wananchi wameishi vizuri. Ukiangalia, utapata mahindi yako sawa, unga uko sawa kwenye maduka na Wakenya hawajalala njaa. Ningependa kumpongeza Rais kwa kuzalisha mazao ya shambani. Jambo lingine ambalo ningependa kumpongeza Rais kuhusu ni mfumo wa"
}