GET /api/v0.1/hansard/entries/1502462/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502462,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502462/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "(JSS) waweze kusoma vizuri. Nikiangalia katika sekta ya ukuzaji wa sukari, tulikuwa tunapata kama tani 40,000. Sasa zimeongezeka na kuwa tani 84,000 ambazo zimetufanya tusiagize sukari kutoka nje. Tunatumia sukari ya hapa nyumbani. Nampongeza Rais kwa juhudi zake. Wajua kila kitu kinachukua muda. Kitu nilichogundua ni kuwa Rais alikuwa pengine hana timu iliyokuwa inaweza kumzungumzia yale mambo mazuri ambayo amefanya. Lakini kwa yote ambayo alituelezea, nimezingatia moja baada ya nyingine na nikaona kuwa si yale wanayoyasema kwenye mitandao kuwa Rais ni mtu mrongo. Hapana. Nampongeza Rais. Hata watu wakikurushia mawe, yachukue uyajengee taifa maanake hata ukifanya kitu kizuri, mtu mbaya siku zote atakutoa aibu wakati umefanya kitu kizuri. Kwa hivyo, ninampongeza Rais kwa juhudi ambazo amefanya. Jambo lingine alilolizungumzia ni femicide ama mauaji ya kiholela ya wanawake. Hilo ni jambo ambalo limetugusa sana akina mama wengi. Hata juzi, niliona huko Nakuru mchungaji wa kanisani aliyemdhuru na kumkata mke wake vibaya sana. Nasi tunajua kuwa kanisa ndilo linafaa liwe mbele katika kuleta amani katika ndoa. Siyo mchungaji huyo tu. Kuna wengine ambao hawako kwenye makanisa lakini bado wanawaua wanawake. Rais alizungumzia jambo hilo na kutuhakikishia kuwa wanawake wa taifa letu watapewa ulinzi. Lakini kama alivyosema mwenzangu, ulinzi unaanza na wewe mwanamke. Usijitoe waziwazi kwenda kwenye mahoteli au Airbnb na humjui mtu unayekutana naye. Anakumalizia huko kisha tunaanza kumsumbua President na mambo yetu ama starehe zetu za kibinafsi. Wanawake tuwe macho na tujichunge sisi wenyewe. Najua kuwa Rais alisahau kuzungumzia mambo ya blue economy, lakini nataka nimpongeze. Waziri wetu ambaye ni mgeni amefanya kazi nyingi na tunaona matunda makubwa sana ya blue economy . Akina mama kule Mombasa wanafanya biashara na wamepata pesa za kufanya biashara. Kwa hivyo, nimpongeza sana Rais."
}