GET /api/v0.1/hansard/entries/1502493/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502493,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502493/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Natoa kongole kwa Hotuba ya Rais Daktari William Ruto. Katika Hotuba yake, alizungumzia mambo mengi sana. Jambo la kwanza, nakubaliana na yeye kwamba shilingi yetu imejizatiti na kufika KSh129 kwa US$ moja kutoka Ksh162. Hii inamaanisha kuwa tunaelekea katika mkondo sawia kiuchumi. Hivyo basi, jambo hili linaweza kuwashawishi sana wawekezaji kutoka mataifa tofauti na wale wanaotoka nchini pamoja na wafanyibiashara. Hivyo, tumeona shilingi yetu imenawiri na kujisatiti juu ya dola. Kwa upande wa Special Economic Zones kama za kule kwangu Likoni, mpaka sasa, takriban wawekezaji 94 wameweza kuleta barua za kusema watawekeza katika sehemu ile. Hii ina maana kuwa uchumi wa taifa la Kenya utaweza kupanuka na ajira zitakuwa nyingi kwa vijana wetu. Mhe Rais pia alizungumzia njia ya kutafuta ajira pasi na zile zilioko katika taifa letu. Tumeona ametafuta ajira katika bara Uropa, Asia na zinginezo. Hili ni jambo nzuri. Lakini kuna wahusika wanamuangusha Mhe. Rais. Nafasi hizo zinavyotokea, hazisambazwi kwa njia ya usawa na uadilifu kwa kaunti zetu 47. Haswa, tukiangalia kuna kaunti kama za kaskazini mashariki, sehemu za Pwani na zile zinginezo, nafasi hizo hazifiki. Hivyo basi, Wakenya wanaona pengine jambo hili halifanyiki, na kumbe linafanyika tena kwa hesabu za juu sana. Wakenya zaidi ya laki moja wameenda kufanya kazi katika nchi za nje. Kwa hivyo, tunasema wahusika waangaliwe waweke ukenya kwa jambo hili. Vile vile, kwa kufufua viwanda vyetu vya sukari, uchumi umeimarika. Pili, tunajenga ajira. Vile vile, tunapunguza gharama ya maisha kwa wakenya kwa sababu bei ya sukari itashuka. Shilingi inavyonawiri, tunaona bei ya bidhaa kama unga na mafuta imeshuka. Kwa hivyo, kuboresha viwanda vya sukari ni jambo nzuri sana. Hivyo basi, tunaomba kiwanda cha Ramisi kule Kwale katika eneo la Pwani kiweze kufufuliwa, kuimarishwa ili uchumi uweze kupanuka. Jambo lingine nataka kulizungumzia ni swala la elimu. Rais alilizungumzia sana swala la elimu. Alisema walimu wengi sana waliandikwa kazi wakati wa awali na hivi sasa pia, walimu takriban 20,000 wataweza kuandikwa kazi. Namwambia Mheshimiwa Rais kuwa tunampongeza kwa jambo hili. Lakini ninarudia kusema kuwa wahusika waweze kusambaza nafasi hizo za walimu katika kaunti zetu 47 ili waone kuna uadilifu na usawa. Kwa Kiingereza, tunasema equity na equality. Maanake, tukizungumzia uadalifu na usawa, ni zile sehemu ambazo zimekuwa na changamoto zipate walimu zaidi. Swala lingine ni lile la Adani. Nampongeza Rais kwa kukomesha sakata hiyo. Kwa sababu lazima uwekezaji ufuate utaratibu na sheria na utumie fedha yenye haitamuumiza mwananchi katika taifa ya Kenya. Jambo lingine ni dhuluma za kijinsia, haswa kwa watoto wetu wa kike. Tumeona watoto wetu wakitekwa nyara na kuuliwa kikatili. Kwa swala hili, vitengo vya usalama na ujasusi lazima vijizatiti ili tuweke usalama kwa akina mama zetu, wasichana na vijana. Jambo la mwisho, alizungumzia kuhusu umoja wa mataifa…"
}