GET /api/v0.1/hansard/entries/1502499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502499/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "kukataaa kwake kunatokana na kusikiliza. Hata hivyo, Mamlaka ya Kusimamia Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) imepewa nafasi tena. Tunataka Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta uwe sawa na viwanja vingine vya ndege, kama vile Doha. Kuna Wakenya wengi kule. Ukiingia Doha, utafikiri uko katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta. Watu wengi wametoka makwao kwa sababu ya shida za kiulimwengu. Ikiwa Airport itaendelezwa vizuri, walio nchini wataandikwa kazi na hata wale watakaotaka kurudi nchini wanaweza kurudi na kufanya kazi nzuri. Kwa hivyo, nataka kuambia KAA kuwa, kwa kuwa President amesitisha Adani, ni lazima wajitahidi Airport iwe nzuri. Mambo madogo madogo yamewashinda kufanya, kwa mfano, ukiingia airport zote Kenya, utakachoona ni jinsi ambavyo taxi zipo na vyoo vilivyo. Ukivitazama tu, utajua ni sura ya Kenya. Vitu vidogo vimewashinda. Ukiangalia vyoo ni vichache na usafi sio wa standard kama zile za viwanja vingine vya ndege. Upande wa taxi, abiria wanavutwavutwa ni kama wako katika Soko la Kongowea, Mombasa. Wenye taxi hawawezi kupanga laini. Niliuliza hili swali wakati mmoja na hata Waziri akaalikwa hapa, lakini hilo la laini halijawahi kufanyika. Sijui sababu ni nini. Mimi hamu yangu kubwa ni airport ibadilike iwe kama airports za mataifa mengine. Huwa tunaambiwa kuwa hapa East Africa, sisi ndio big brother. Lakini airport zetu zinatoa sura mbaya ya Kenya. Nilipendezwa na hutuba ya Rais na ninampongeza kwa mengi aliyosema. Rais kwa kweli anafaa kupewa muda. Ana nia nzuri ya kuiendeleza nchi hii. Akipewa muda, atatekeleza na mambo yatabadilika. Rais alizungumza kuhusu madeni ya kitaifa kuwa mengi alipoingia uongozini. Hata hivyo, hakuongeza madeni. Alitumia hekima. Angeongeza madeni, tungepigwa mnada kama nchi zingine. Inafaaa Wakenya waangalie jinsi ambavyo haya mambo yanavyoenda. Wasiwe tu wakiweka lawama. Sasa hivi, Rais ametuliza taifa na wakenya wamefurahi. Rais alizungumza juu ya kupunguza matumizi na ubadhirifu katika Speech yake. Hilo ni jambo nzuri ambalo Wakenya walitaka kulisikia. Kusema ukweli, Kenya inajiweza. Huwa inaporwa lakini bado husimama. Jee, ikiwa haitaporwa, si Kenya itakuwa mbali zaidi? Rais alizungumza juu ya bei ya bidhaa kupungua na ni ukweli bei zimepungua. Ukweli unafaa kusemwa. Kuna bidhaa kama unga ambazo zilikuwa ghali na kwa sasa bei yao imerudi chini. Kwa hilo, tunafaa kumpongeza Rais. Mtu akifanya mema, aambiwe amefanya mema. Kama wenzangu walivyo zungumza, shilingi ya Kenya imepata thamani dhidi ya dola. Ilivyokuwa awali ni tofauti na sasa. Wanaofanya biashara wameona utofauti huo. Hapo ninampongeza. Suala la kuwaandika waalimu kazi ni jambo nzuri. Maeneo bunge yetu hufanya mitihani sawa na maeneo bunge mengine. Hayafanyi mitihani tofauti. Shule ya upili ya Siyu ilikuwa ya mwisho kule Lamu East. Hata hivyo, tatizo halikuwa la shule. Wanafunzi hawajawahi kumwona mwalimu wa chemistry tangu shule hiyo ijengwe. Watatatuliwa vipi? Naomba waalimu waandikwe. Najua tuko kwa mpangilio katika Serikali hii. Kitakachopatikana tutakipata. Kwa afya, sisi kama Wabunge tutie bidii ili watu wetu wajiandikishe katika mpangilio wa bima ya afya. Ni mpangilio mzuri na utawasaidia sana Wakenya. Kuhusu nyumba, huo ni mpangilio mzuri. Nyumba zitasaidia na itakuwa legacy ya Rais…"
}