GET /api/v0.1/hansard/entries/1502540/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502540,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502540/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Kwanza, nizungumzie swala la Adani. Kwa kuivunjilia mbali kandarasi ya Adani, Mhe. Rais amefurahisha Wakenya wengi kwa sababu ni jambo ambalo lilikua limeleta utata mkubwa. Wafanyikazi wote walikuwa na wasiwasi kwamba badala ya kulipwa kwa mwezi, watabadilishwa kuwa na mikataba. Ni jambo la utata mkubwa kuona rasilimali yetu tunayoitegemea, mtu akikuja kuisimamia kwa miaka 30. Kwa hivyo, ilikua ni wasiwasi mkubwa. Alipoifutilia mbali, amefanya jambo nzuri. Amesikiliza wananchi, na kiongozi yeyote ni yule anayesikiliza wananchi. Kwa hivyo, hilo nampongeza Mhe. Rais."
}