GET /api/v0.1/hansard/entries/1502541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502541/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Nikija katika upande wa shilingi kuwa na nguvu, ni kweli, shilingi yetu ilikuwa imekosa thamani kubwa. Hata ilikuwa ukienda kwa nchi jirani kubadilisha pesa yetu ya Kenya wanaikataa. Wanasema pesa ya Kenya haieleweki kwa maana leo iko hivi, kesho iko chini zaidi. Lakini imeimarishwa na mpaka sasa pesa yetu inaheshimika. Kushuka kwa dola, sisi tunategemea kwamba taifa litaimarika wakati pesa za kigeni na hali ya uchumi kama mafuta yataweza kushuka bei. Isipande kwa sababu dola imeanguka. Kwa hivyo, wananchi wanategemea wakati dola imeendelea vizuri na pesa zitashuka ili kusudi mwananchi aweze kujikimu ama gharama za maisha zisiweze kupanda juu."
}