GET /api/v0.1/hansard/entries/1502542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502542,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502542/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Tuje katika upande wa SHA. Mimi mwenyewe nimeweza kushuhudia wagonjwa wa moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mombasa, yaani Coast General Hospital . Kuna mgonjwa ambaye alienda kuwekewa pacemaker au kifaa ambacho kinaweza kufanya moyo wake upige kwa usawa, bill yake ikaja Ksh1.3 milioni. Na nikashangaa kuona SHA imemlipia Ksh1.1 milioni papo hapo. Kwa hivyo, nimeona ni jambo ambalo kama watalitilia bidii; kama hawatabadilika, hii SHA itasaidia sana mwananchi wa kawaida. Na vile vile, ukiangalia SHA katika levels 2, 3, 4 hospitals, ukipiga tu kwenye simu yako *147# ili kujisajili, wewe unatibiwa bila malipo. Ikiwa itaendelezwa vile inavyoendelea sasa, itawasaidia mwananchi wa chini kwa ukubwa sana."
}