GET /api/v0.1/hansard/entries/1502543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502543/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Hivi sasa, SHA kwa mwezi ni shilingi Ksh300, NHIF ilikuwa Ksh500. Kwa hivyo SHA kwa mwaka ni Ksh3,600. Nina imani kwamba ikiwa watajipanga vizuri, itakuwa jambo la busara kwa sababu matibabu ni ghali sana na mwananchi wa kawaida hawezi kulipa. Katika NHIF, kulikuwa na uzito mmoja. Wakati unaambiwa unangoja approval, unaweza kungoja masaa matatu au matano kabla kupewa hiyo ruhusa ya kupewa dawa ama kuruhusiwa kwenda nyumbani. Lakini SHA kwa sasa ni kwamba ukingoja approval, hauchukui muda. Kwa hivyo, ikiwa wataendelea namna hii, basi itasaidia wananchi sana. Juzi tu nimetembelea hiyo hospitali na SHA wamelipa kufikia sasa Ksh21.9 milioni kwa wagonjwa wa moyo. Tunaipongeza SHA kwa kufanya hivyo. Itilie mkazo na iongozwe na watu ambao wataweza kuiendeleza zaidi."
}