GET /api/v0.1/hansard/entries/1502656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502656/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa hii nafasi. Kwanza, ninashukuru kamati iliyokaa chini na kuhakikisha wamefanikisha maelewano kati ya fedha ambazo zinaenda kaunti zetu. Kazi inayofanywa na Maseneta ni muhimu sana. Shida ambazo wanapitia kuhakikisha kwamba pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu zimefika ni kazi ngumu, ni kazi msalagambo. Ni kazi inayohitaji Maseneta kumakinika na kutetea gatuzi zetu. Bw. Naibu Spika, jambo la ajabu ni kwamba hizi fedha zinapofika katika kaunti zetu, magavana wengi wanajifanya kama miungu na hawawezi kulizwa maswali. Ni kama Seneti tumekuwa tingatinga; kazi yetu ni kuchukuliwa kubomoa milima na tunapomaliza kutengeneza barabara na fedha kufika kaunti zetu, inasemekana tutaharibu barabara na lazima tuwekelewe kwa lori. Bw. Naibu Spika, ile pesa tumeng’ang’na leo na kuhakikisha kwamba imepita, ningeuliza wale magavana ambao wanatumia hizi pesa, wazitumie kwa njia ya haki, kuhakikisha ya kwamba kuna maendeleo mashinani. Nitasema hivi, Mswahili husema ukitaka kujua chochoro, kula nauli. Sisi kama Seneti, tumemakinika na tutahakikisha kwamba kuanzia mwaka ujao, tutafatilia fedha zetu zinaenda wapi. Ukiangalia mahospitali katika gatuzi zetu, utapata watu wetu bado wanahangaika kwa sababu ya ukosefu wa madawa na huduma muhimu. Utasikia gavana akisema anang’ang’ana na barabara na elimu. Hiyo ni sawa, lakini ni vizuri wajue afya ya wananchi wetu ni muhimu zaidi. Kwa sababu, aliyekufa, hawezi tumia barabara au basari. Bw. Naibu Spika, Seneta Cherarkey anaongea kwa sauti ya juu na ananipotezea mtiririko wa mawazo ninapoongea."
}