GET /api/v0.1/hansard/entries/1502659/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502659,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502659/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ni vizuri niseme ya kwamba, miradi mingi ambayo inafanyika katika gatuzi zetu ni kama magavana wengi wamesahau kuna ukulima na uvuvi. Katika nyanja ya uchumi samawati, shida iliyoko ni kwamba, ukiangalia zile bajeti zinatengenezwa na kupelekwa bunge zetu za kaunti, huwezi pata hata moja imewekwa pesa za kutosha kwenda kwa uchumi samawati. Tumetembea sehemu mbalimbali kule uvuvi unafanyika na cha kushangaza ni kwamba, wavuvi bado wanahangaika na bado kuna fedha zinafaa ziende kusaidia wale wavuvi. Bw. Naibu Spika, mkulima ni mtu wa maana na nitaregea kusema kwamba kama kuna mtu anahitajika katika maisha ya kila siku ni mkulima. Tunahitaji mkulima asubuhi wakati tunatafuta staftai, chakula cha mchana na hata jioni, mara nne kwa siku. Lakini wakulima wengi wamewachiliwa na tunajua ya kwamba, kilimo imegatuliwa. Kwa miaka yangu ya awali, nimekuwa mwakilishi wadi katika gatuzi la Kirinyaga na nikawa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kirinyaga. Gavana wangu ni yule aliopo leo na utapata kwamba zile fedha zimewekwa hususan kwenda kwa wadi kwa sababu wadi ni sehemu ndogo sana ya ugatuzi. Bw. Naibu Spika, wabunge kutoka kaunti ya Kirinyaga wanang’ang’ania miradi ambayo wamepeana kupitia kwa magavana kuweza kutekelezwa. Wabunge wanakuwa maadui wa gavana. Njia tunayoweza tumia kuhakikisha kwamba fedha mbazo zinafikia magavana zimefika kwenye kona zote za magatuzi yote 47 ni kuhakikisha kwamba miradi ambayo imepeanwa na waakilishi wadi wote inatekelezwa katika wadi ambazo wanasimamia. Uongozi si mapenzi. Sio lazima gavana awe anasikizana na mwakilishi wadi ama Seneta. Katika siasa hata kama hampendani, ni lazima huduma ifikie mwananchi. Kukosana katika kazi sio neno kwa sababu mwishowe tunafaa kufanya kazi. Jana Kamati ya Uwekezaji wa Umma na Hazina Maalum za Kaunti ilikuwa na kikao na gavana wa kaunti ya Kirinyaga. Ajenda ya mkutano ilikuwa maswali kuhusu iliyokuwa kampuni ya Kirinyaga Water and Sanitation Company (KIRIWASCO) ambayo ilikuwa inahusika na maji. Hadi hivi sasa, fedha ambazo zinakusanywa na KIRIWASCO hazijapitishwa vilivyo katika bunge la kaunti ili iweze kugawiwa majukumu kulingana na sheria ambayo inahusika na ununuzi wa bidhaa. Bado kuna mashimo mengi ambayo pesa zinazookotwa katika kaunti zinapotelea. Kwa hivyo, magavana hawafai kulia kila siku kwani pesa haitoshi. Tunataka kuona pesa inayokusanywa mashinani ikikusanywa kwa njia inayofaa, kwa uaminifu na kufikia malengo ambayo inafaa. Jambo la mwisho ni kuhusu eneo la Mwea ambalo ni eneo kubwa linalokuzwa mpunga katika eneo la Kirinyaga. Wakulima wengi wanahangaika. Kwa sababu, ingawa kuna mbolea ya ruzuku, pembejeo ambayo imefikishwa na kufanya wakulima waongeze mazao bado kuna tatizo kubwa kwa miundo msingi ya kutoa mazao yao kutoka mashambani kufikishwa kwa maghala. Tunazalisha mazao mengi, lakini wakulima wanapoteza mazao mengi shambani. Gharama ya kutoa gunia moja ya mpunga kutoka mashambani kupeleka katika maghala ya National Cereals and Produce Board (NCPB) na vyama vya ushirika katika eneo la The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}