GET /api/v0.1/hansard/entries/1502660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502660/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Mwea. Hii inagharimu wakulima shilingi 1,200 katika kila gunia. Kama mkulima atapoteza shilingi 1,200 kwa sababu ya miundo msingi ambayo inafaa itengenezwe na gatuzi ya Kirinyaga, inamaanisha kuwa ile faida yote inapatikana kwa sababu ya kupata mbolea ya ruzuku na pembejeo za bei ya rahisi inapotea. Ningependa kumwambia gavana wangu kuwa mghala muue na haki yake umpe. Tuhakikishe kwamba huduma za barabara na miundo msingi imeboreshwa ili wakulima waweze kufaidika. Sio haya tu ambayo nilikuwa nataka kusema siku ya leo. Najua kwamba kamati nyingi zimekuwa na matatizo kubwa wakati tunawaita magavana hapa kuja kujibu maswali. Mswahili husema Mrina haogopi nyuki. Kama unataka asali lazima utafuata mzinga na kuzoa asali uwe unaumwa na nyuki ama huumwi na nyuki. Unapoomba kiti cha gavana, lazima uwe tayari kukaa chini na wale ambao wanaangalia kama kazi inafanyika katika gatuzi. Lazima uwe tayari kukaa chini na kujibu maswali kwa wale waakilishi wadi ambao wamechaguliwa. Lazima kuwe na heshima kuhakikisha kwamba kila jambo ambalo unafanya, unawajibika. Nitakuwa kalili wa akili kama sitasema kuwa kumekuwa na madharau si haba kutoka kwa magavana, waakilishi wadi na Maseneta ambao walichaguliwa. Itafika siku ambayo tutakuwa na kikao. Kazi yetu sio kubeba mzigo mkubwa na wakati tunawauliza maswali wanatuambia mzigo uko kichwani. Lazima waajibike kwa kujibu maswali na kufanya kazi ambayo wamepewa kufanya na isiwe kazi yao ni kutupatia kazi ya kuwatafutia pesa lakini hawataki kujibu maswali. Asante, Bw. Naibu Spika."
}