GET /api/v0.1/hansard/entries/1502683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502683,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502683/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nataka kumfahamisha rafiki yangu Sen. Karungo Thang’wa, Seneta wa Kaunti ya Kiambu, kwamba Raisi wa Kenya hakuwa kwa Kamati ya Usuluhishi. Kamati ya Usuluhishi ilikuwa na Maseneta tuliowachagua hapa pamoja na Wabunge ambao hawapendi kusikia kaunti zetu zikipata hela inayofaa. Nakosoa rafiki yangu, Sen. Karungo Thang’wa, kwamba hakuna mahali Rais alihusika kwa sababu kuna demokrasia. Aliruhusu Kamati ya Usuluhishi ikae chini ili kaunti zetu zipate hela inayofaa; shilingi 400 bilioni. Angekosoa Kamati ya Bunge ambayo haitaki ugatuzi ufanye kazi. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}