GET /api/v0.1/hansard/entries/1502695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502695,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502695/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "yalikuwa ni majadiliano kulingana na vile ambavyo hatukuwa tumeelewana katika ugavi wa pesa zinazoenda kwenye serikali zetu za mashinani. Majabali wetu waliokuwa katika hii Kamati wakiongozwa na Sen. Ali Roba, walikuwa Sen. Sifuna, Sen. Murgor, Sen. Faki, Sen. Veronica Maina, Sen. Onyonka, Sen. Wamatinga, Sen. (Prof.) Tom Ojienda Odhiambo, SC, Sen. Mungatana, na Sen. Oketch Gicheru. Tuliwapeleka majabali hawa ambao walifanya bidii walivyoweza kujadiliana na kupitisha pesa zile. Kulingana na matokeo ya awali tulikuwa tumesema tupeleke Shilingi 400 bilioni kwenye serikali za kaunti 47 zote. Wagawanye taratibu ili kila kaunti ifaidike na zile pesa. Lakini kwa sababu ya sintofahamu tofauti katika Bunge la Kitaifa, walionelea hizi pesa zipunguzwe. Lakini hawa majabali wetu ambao tulichagua hapa walifanya bidii na hatimaye wakafikisha kiwango cha Shilingi 387 bilioni ambacho si kiwango kibaya kulingana na tunavyoelewa kuwa asilimia 15 ndio sheria inaruhusu. Kipengele 96 cha Katiba ya Kenya, kinasema kwamba kazi ya Seneti itakuwa kulinda na kutetea kitita cha pesa ambacho kitapelekwa katika serikali zetu za mashinani. Hii ni kazi muhimu sana katika Bunge hili la Seneti. Hakuna mwaka tutaketi bila kupeleka pesa hizi katika serikali zetu za gatuzi. Lakini ijapokuwa zimepungua, huo ndio wajibu ambao tunataka. Magavana wanafaa kuketi chini na kufikiria jinsi wataweza kutumia hizi pesa ambazo zimepunguzwa ili kuendeleza maendeleo katika serikali zetu za mashinani. Bw. Spika wa Muda, hakuna mtu anayeweza kufaulu kutekeleza maendeleo ikiwa hatapata pesa na ndio maana nasisitiza umuhimu wa kipengele hicho. Nawapatia kongole Maseneta wote kwa kutia bidii kuona kuwa Shilingi 387 bilioni zimetengwa kuenda kwa serikali zetu za mashinani ili kuendeleza maendeleo. Kongole ndugu zangu katika Bunge hili la Seneti. Vile vile, nakubaliana na Ripoti hii ambayo imeundwa kwa taaluma ya hali ya juu. Baada ya pesa hizi kufikia magavana, hawafai kuona kama wao ndio wakubwa ila wanafaa kuelewa kwamba wao ni watumishi wa wale waliowapigia kura. Kwa hivyo, tungetaka utumishi ubainike wazi ya kwamba hizi pesa ambazo tumepeleka katika serikali zetu za mashinani zinatumika kwa hali inayofaa. Tunajua kuna ufujaji wa pesa kwa njia tofauti tofauti lakini pesa hizi zikitumika vyema wale wananchi wa mashinani watafaidika. Hii ndio sababu na umuhimu mkuu wa kupeleka hizi pesa kwenye serikali zetu za mashinani. Ni lazima tuone ya kwamba magavana, maspika wanaohusika kusambaza hizi pesa wamezitumia kwa njia ya nidhamu. Matumizi katika hospitali; tunasema hospitali ni kiwango cha kwanza, maanake katika kaunti, hakuna kaunti itakuwa na mwelekeo mwema ikiwa watu wake wengi watakuwa ni wagonjwa. Tunataka afya za Wakenya wanaoishi nchini ziwe sawa sawa. Jukumu hili sasa limepelekwa katika serikali za mashinani ili kuona ya kwamba wale watu wanaowaongoza katika serikali za mashinani wako na afya njema. Hii ndiyo sababu kubwa tunasema kwamba ni lazima kitengo kikubwa sana cha hizi pesa zinazokwenda katika serikali zetu za mashinani ziende katika hospitali zetu. Pesa hizi zitaweza kutumika kwa kuchukuwa madawa na vifaa ambavyo vinaweza The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}