GET /api/v0.1/hansard/entries/1502696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502696,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502696/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "kuhudumia mtu aliyepata ajali ama mtu anayetaka kulazwa katika vile vyumba ambavyo vinaitwa Intensive Care Unit (ICU) au chumba cha wagongwa mahututi; chumba ambacho mtu anaweza kupata madawa na hatimaye akatoka katika ile hali yake ya kimahututi na akaja akiwa mzima tena na akarudi kwa jamii yake akiwa na afya njema. Tunasema hiyo ndiyo sababu tunasisitiza sana kwamba pesa nyingi zipelekwe kwa hospitali ili wakenya wawe na afya nzuri, nchi itakuwa na maendeleo zaidi. Bw. Spika wa Muda, vile vile kuna hali za mawasiliano. Pesa hizi si za kutumia vile mtu anavyotaka, ila tuone hali za mawasiliano. Barabara zile za mawasiliano zinazokwenda katika vijiji vyetu vya vitongoji tunasema hizo pia zitengenezwe. Hizi pesa ambazo tumezipeleka hivi sasa ziko katika mikono ya magavana ili waweze kuzitumia kuona ya kwamba kutakuwa na barabara njema ya usafiri au hali ya maisha kutoka pointA to point B kwa w ananchi wa Kenya imeimarishwa. Vile vile, inajulikana kwamba uti wa mgongo wa nchi hii ni ukulima. Tunajua kuna wakulima katika sehemu mbali mbali ya nchi hii. Wengine pengine katika sehemu za kaskazini ya Kenya ni watu ambao wanategemea mifugo. Tunasema tuweze kupeana kipaumbele kwa huduma za wale watu wanaotoka maeneo tofauti tofauti. Kama sasa watu wa North Eastern, watu wanaoketi kule wanataka ng’ombe, ngamia na mahitaji fulani fulani. Tunaona ya kwamba lazima gavana wa upande huo atilie mkazo mambo haya. Tukija upande wa kilimo, kuna sehemu tofauti tofauti za Kenya ambako kuna wakulima. Tunataka pia hizi pesa zitakazoenda kwa serikali zetu mashinani, magavana waweze kuzingatia wakulima na kuwapa kipaumbele. Hii itawawezesha kuwa na mashamba yao ambayo wataweka rotuba, fertilizer na mbegu ili wapate chakula kingi. Hakuna nchi ambayo inaweza kufaulu, bila kuhakikisha chakula kinapatikana ili watu waweze kushiba, kufanya kazi kwa bidii ili kuwe na maendeleo. Tunaiita food security . Mara nyingi, tumeona watu waliosimama au wanaopinga na hatuwakatai. Kupinga ni sawa, lakini Ripoti hii imetengenezwa na Kamati. Hii Ripoti ni ya Kamati si ya Rais. Tukiketi hapa kama Maseneta na tukianza sintofahamu ya kwamba tunaongea juu ya taarifa aliyoitoa Rais ya mwaka wa 2024 katika hili Bunge letu, tukiileta hapa na kuifananisha na hii Ripoti, haitakuwa sawa. Tutakuwa tumekosa mwelekeo. Ripoti ya Rais iko kando na Ripoti hii ambayo imetengenezwa na Kamati yetu ya majadiliano katikati ya Mabunge yote mawili. Walikubaliana na hizi pesa na tunaongea habari za pesa zitakazoenda katika serikali za mashinani ili ziweze kusaidia wananchi wa Kenya. Nikimalizia, ningependa kuongea na wafanyikazi wanaofanya katika serikali zetu za mashinani. Wazungu walisema ya kwamba, na uniruhusu nitumie lugha ya kimombo, “ your first client is your employee and a happy worker is a productive worker.” Kitu cha kwanza ambacho magavana wanatakikana kuona ni kwamba wale wafanyikazi ambao wameandikwa ndani ya maofisi zao wameangaliwa. Tunashangaa ya kwamba sasa kuna sababu ndogo ndogo ambazo tunaweza kuziona zikitoka kila mahali katika Kenya kwamba wafanyikazi wamekosa mishahara. Tunasema hakuna anayetaka kufanya kazi na baada ya siku thelathini asione mshahara wake ndani ya mfuko ili aende nyumbani akifurahi, kuweza kulipa karo za watoto wake, kulisha bibi yake na kuwavisha pamoja na watoto ili nyumba ile iwe na raha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}