GET /api/v0.1/hansard/entries/1502697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1502697,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502697/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Tunaona simanzi zinatandaa katika familia tofauti tofauti kwa sababu ukiulizwa unasema mimi sina pesa za kulipa mishahara. Lakini sasa hakutakuwa na sababu ya wafanyikazi wetu wanaofanya kazi katika serikali za mashinani kukosa mishahara yao. Nasema kwamba kipaumbele iwe ni wafanyikazi wenu wanaofanya kazi katika kaunti zote 47 katika Kenya. Hivi sasa pesa ziko. Walipeni mishahara yao. Bw. Spika wa Muda, nataka kumalizia kwa kusema hii Ripoti yetu tuliiandika na kukubaliana nayo. Hii ni kwa sababu ni ripoti ambayo imepeana mwelekeo na imeeleza ni sababu gani tumeweza kukubaliana kuchukua hizi Shilingi 387 bilioni. Tukakubali zile zingine kama shilingi 13 bilioni zipotee lakini hali ilivyo ni kuwa hali ya uchumi nchini si nzuri. Hata hivyo, sisi tunawaombea hao magavana waweze kuketi katika yale maofisi. Waweze kukaa chini, kutafakari na kuona ya kwamba maji yatasambazwa, barabara zitapatikana na mbegu zitapelekwa kwa wakulima, hospitali zitakuwa na madawa na hatimaye pia mishahara ya wafanyikazi katika serikali zetu za mashinani itapatikana kulingana na uwezo na nguvu zao. Wasifanye kazi wakijipiga vifua halafu mishahara isipatikane. Kwa hivyo, tunasisitiza katika hii Ripoti naunga mkono kwa sababu ni ripoti ambayo imetengenezwa na Maseneta wenzetu. Wameileta hapa na sisi tunaona ya kwamba ripoti hii itasaidia vilivyo katika serikali za mashinani. Asante."
}