GET /api/v0.1/hansard/entries/1502699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1502699,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502699/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa niweze kuchangia Ripoti hii kuhusu hela zinazoenda katika kaunti zetu. Naunga mkono Ripoti hii ambayo inaonyesha vile pesa zitaenda mashinani. Ingawa pesa hizi hazitoshi kwa sababu nakumbuka mwaka jana, kaunti zote 47 tulipitisha Shilingi385 bilioni, lakini mwaka huu kabla mambo ya budget tukapitisha Shilingi400 bilioni ambazo tulidhania itasaidia watu mashinani. Walakini, iliporudi huku baaada ya budget kuanguka, National Assembly walisema Kaunti zote 47 watapatiwa Shilingi380 bilioni. Hii ina maana kuwa walipunguza Shilingi bilioni tano. Maseneta nao waliona hiyo haifai na ndio tukaunda Kamati ya Mediation na tukachagua Maseneta tuilioona wanafaa kwenda kwa kikao na wale wa Kamati ya Budget ya National Assembly. Walipokaa, waliongeza kutoka kwa Shilingi380 bilioni mpaka Shilingi385 bilioni. Sasa tunaona ni kama waliongezea Shilingi bilioni mbili ikawa Shilingi 387 bilioni. Kwa hivyo, naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}